LIGI YA ATAWAS MAJI CUP KANDA YA ZIWA NAMBA TATU YAHITIMISHWA SHINYANGA,TIMU TANO ZA MPIRA WA MIGUU ZAFUZU KUSHIRIKI LIGI HIYO DODOMA
Na Marco Maduhu,SHINYANGA
LIGI ambayo imeandaliwa na Taasisi ya watoa huduma za Maji nchini (ATAWAS) Maji CUP,imehitimishwa huku Timu Tano za Mpira wa Miguu Kanda ya Ziwa namba Tatu zikifuzu kushiriki Ligi hiyo Kitaifa Dodoma, ambapo Timu Nne ni kutoka Mamlaka za Maji,na Timu Moja ya Jamii.
Ligi hiyo inashirikisha Timu za Mamlaka za Maji kutoka Kanda 10 pamoja na Timu za Jamii,ambapo kuanzia Jana hadi leo ilikuwa ni Michezo kutoka Kanda ya Ziwa Namba 3 ili kupata Timu Nne za Mamlaka za Maji na Timu Moja ya Jamii ambazo zitakwenda kushiriki michezo hiyo Dodoma Septemba mwaka huu pamoja na Timu mbili za Mpira wa Pete ili kupata mshindi katika Timu 32 kutoka Kanda zingine.
Mtendaji Mkuu wa ATAWAS Costantino Chiwaligo, akitangaza Matokeo amesema katika Mshindano hayo zilipaswa kushiriki Timu Saba za Mamlaka za Maji, lakini ambazo zimeshiriki Ligi hiyo ni Timu Nne, huku Timu Tatu zikishindwa kushiriki, na hivyo kusababisha Timu Nne kufuzu Moja kwa Moja kwenda Jijini Dodoma.
Amezitaja Timu za Mamlaka za Maji ambazo zimefunzu kwenda Dodoma, kuwani KASHWASA,SHUWASA,MAUWASA na MWANHUZI,huku Timu za Jamii ni Polisi Jamii ambayo itashiriki mashindano hayo Dodoma.
“Timu ambazo hazijashiriki Ligi hii ya Maji Cup kwa upande wa Kanda ya Ziwa namba Tatu ni KUWASA,KISHAPU na BARIADI, na Timu za Pete ambazo zitakwenda Dodoma ni SHUWASA na Mwanhuzi,”amesema Chiwaligo.
Aidha, ametaja Mshindi wa Jumla katika Mashindano hayo kwa upande wa Kanda ya Ziwa namba 3, kuwa ni KASHWASA, Wapili Polisi Jamii, Watatu Ibadhi na Wanne SHUWASA.
Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Shinyanga (SHUWASA)Mhandisi Yusuph Katopola, amewapongeza washindi wote katika michuano hiyo, na kuwataka wajiandae vizuri sababu Dodoma kutakuwa na Ushindani Mkubwa.
Katika uhitimishaji wa Ligi hiyo Timu za Jamii zilipewa Zawadi ya Mipira,ambazo ni Ibadhi,Polisi Jamii,na Shinyanga Veterani Academic.
Lengo la Ligi hiyo ya ATAWAS Maji Cup ilikuwa ni kufikisha ujumbe kwa Jamii, Juu ya kutunza vyanzo vya Maji,Miundombinu ya maji na kuzuia upotevu wa Maji.
Kauli Mbiu katika Ligi hiyo ya ATAWAS Maji Cup 2024,inasema Thamani ya Maji kwa Uhai na Maendeleo.
Timu za Jamii zikipewa Zawadi ya Mipira.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464