Header Ads Widget

WATOTO NA VIJANA KUNUFAIKA NA MRADI WA USAID KIZAZI HODARI




Na Mapuli Kitina Misalaba

Watoto na vijana chini ya umri wa Miaka 17 kuendelea kunufaika na mradi wa “USAID Kizazi Hodari” unaotekelezwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) katika Mikoa tisa (9) Nchini kwa ufadhili wa shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID).

Hayo yamebainishwa na mkurugenzi mshiriki anayesimamia matokeo na asasi zinazotekeleza mradi wa “USAID Kizazi Hodari” Kanda ya Kaskazini mashariki Bwana Aminiel Alten Mongi kwenye kikao cha tathmini ya utekelezaji wa mradi huo leo Juni 27,2024 Mkoani Shinyanga.

Amesema mradi huo pamoja na mambo mengine umelenga kuboresha Afya, ustawi na ulinzi wa watoto walio katika mazingira hatarishi na vijana chini ya Miaka 18 ili kutokomeza maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.

“Mradi huu unafadhiliwa na shirika la maendeleo ya kimataifa la Marekani USAID ambao ndio wafadhili wakuu wa mradi huu na mradi unatekelezwa na makao makuu ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mradi huu unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) ikiwa na jumla ya Halmashauri 41 Mikoa hiyo ni Tanga, Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Singida, Dodoma, Mwanza, Geita pamoja na Mara”.

“Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha Afya, ustawi na ulinzi wa watoto waliokatika mazingira hatarishi na vijana kuanzia umri wa Miaka 0 hadi 17 ili kufikia malengo ya kidunia ya kupambana na virusi vya UKIMWI, 

"kwa maana wale wenye maambukizi waweze kujua hali zao za maambukizi lakini pia wale ambao wamefahamu hali zao za maambukizi waweze kuunganishwa na vituo vya tiba na mafunzo kwa ajili ya kuanzishiwa dawa lakini pia wale ambao wameanzishiwa dawa kufika kwenye vituo ili kufubaza maambukizi ya virusi vya UKIMWI”. amesema Mongi

Mongi amesema makundi yanayofikiwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo ni pamoja na watoto walioathirika na viruri vya UKIMWI, watoto wa wanawake walioko katika mazingira hatarishi pamoja na watoto walioathirika na matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia ambapo amesema kupitia mradi huo watoto wanapata huduma mbalimbali zikiwemo za kiafya.

Ameeleza zaidi kuwa zipo afua mbalimbali ambazo zinalenga kuwaimarisha kiuchumi walezi wa watoto pamoja na mabinti au wanawake walio katika umri mdogo kwenye ngazi ya kaya huku akitaja shughuli zingine zinazofanyika ambazo zinagusa sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu.

“Lakini kuna maeneo ambayo tunayalenga katika utoaji wa huduma ikiwemo suala la Afya tunahakikisha walengwa wanakuwa na Afya bora ambapo pia tunatoa huduma ya bima za Afya ili waweze kupata matibabu pale wanapokuwa wagonjwa lakini pia kupewa elimu ya Afya ya uzazi na huduma zingine lakini pia kuna huduma ya elimu tunahakikisha wanafunzi wanahudhuria shule na tunafuatilia matokeo yao shuleni lakini pia tunawapa vifaa vya shule, pia kupitia mradi huu tunawasaidia mfano kuwapa elimu ya biashara elimu ya fedha yaani kuweka na kukopa pamoja na vifaa anzishi vya biashara ili waweze kuanzisha biashara ndogo ndogo na hapa tunalenga kwenye suala la endelevu wa mradi lakini pia kuna nyanja ya ulinzi na usalama ambapo tunahakikisha kuwa tunawalinda hata kwenye matukio ya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia tunawasaidia ili waweze kubaki kuwa salama”.

“Tulikuwa na malengo ya kuwafikia wanufaika lakimoja na elfu 57, 110 lakini kufikia Mwezi wa tatu ambayo ni tathmini ya nusu Mwaka tumeweza kuwafikia lakimoja 57 elfu 974 ambayo ni sawa na asilimia 105 lakini pia tulikuwa na malengo ya kuwafikia wanufaika katika shughuli za kiuchumi ambapo tulilenga kuwafikia watu elfu 59,162 lakini kufikia Mwezi wa tatu katika kipindi cha nusu Mwaka tumewafikia watu 62, 132”.amesema Mongi

Akizungumza mchumi mkuu idara ya Afya, lishe na ustawi wa jamii kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Bwana Rashid Kitambulio amesema serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la KKKT katika kufikia malengo yaliyokusudiwa huku akishukuru kwa mradi huo wa USAID kizazi hodari ambao unaendelea kuwanufaisha wahanga hasa wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

“Tunashirikiana na Kanisa la KKKT kuhakikisha kwamba shughuli ambazo zimepangwa kufanyika zinafanikiwa na ushiriki wetu mkubwa upo katika eneo la usimamizi ambapo tunahakikisha kwambwa wale walengwa wanapata zile huduma zilizokusudiwa lakini eneo lingine tunashirikiana katika kuzipitia taarifa za utekelezaji wa mradi huu, tukiangalia moja ya mafanikio ni kwamba hizi jamii ambazi zilikuwa zimesahaulika kwa sasa hivi tumeweza kuzibaini kupitia mradi wa USAID Kizazi Hodari na tunashukuru walengwa wanaendelea kunufaika”.amesema Kitambulio

Kwa upande wake mganga mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu amesema mradi wa USAID kizazi hodari umekuwa na manufaa makubwa hasa katika sekta ya Afya ambapo pamoja na mambo mengine baadhi ya familia wamepatiwa ufadhili wa kadi za bima ya Afya ICHF ambapo amesema kandi hizo zimekuwa zikiwasaidia katika kupata matibabu watoto na familia kwa ujumla.

Naye mratibu wa Mikoa na Halmashauri kutoka tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) amepongeza kwa mradi huo kuendelea kuwatambua na kuwawezesha kupata huduma zinazistahili waathirika wa virusi vya UKIMWI ambapo ameshauri mradi huo wa ‘USAID Kizazi Hodari’ kuwa endelevu ili kuzuia maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.

Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) mradi wa ‘USAID Kizazi Hodari’ limeitisha mkutano wa wadau wanaoshiriki katika utekelezaji wa mradi huo wakiwemo wawakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya maendeleo ya jamii, jinsia wanawake na makundu maalum, TACAIDS, kamati ya usimamizi wa Afya ngazi ya Mikoa na Halmashauri, wadau wanaosimamia afua za tiba na mafunzo katika Mikoa husika ili kupitia na kutathimini utekelezaji wa shughuli za mradi na kuweka mipango endelevu ya mradi huo.


Mratibu wa Mikoa na Halmashauri kutoka tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Amina Masood akizungumza leo Juni 27,2024.






Post a Comment

0 Comments