Header Ads Widget

HALMASHAURI ZA MKOA WA SHINYANGA ZAWASILISHA TATHIMINI YA PJT-MMMAM KULINDA WATOTO


Wadau wa kikao cha PJT-MMMAM mkoani Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja.

Na Kareny Masasy,Shinyanga

HALMASHAURI sita za mkoani Shinyanga zimepitia tathimini za utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa(ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM ) ili kufikia ukuaji timilifu wa watoto kuanzia Umri Sifuri hadi Miaka Nne.

Akifungua kikao cha tathimini tarehe 19,June,2024 Mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga DK Yudas Ndungile amesema lipo jukumu la wadau wote kumlinda mtoto kuanzia akiwa tumboni na hata akizaliwa aweze kulelewa katika nguzo tano zilizoainishwa za lishe,afya,Ulinzi na Usalama,Ujifunzaji wa awali na uchangafu.

Dk Ndugule amesema watoto watakapo lelewa kwenye msingi inayotakiwa itawezekana kuwapunguzia mzigo jeshi la polisi katika suala la uhalifu kwani wanatakiwa waanze kulelewa wakiwa bado wadogo na kupewa maadili.


Afisa Ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lyidia Kwesigabo amesema katika maazimio matano waliyojiwekea watahakikisha wanayafanyia kazi na kuyaboresha yale yaliyoonekana yana mapungufu ikiwemo kuwapa wadau nao kuwasilisha maoni yao kwa kipindi kijacho.

Maafisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri zote waliwasilisha tathimini katika maeneo yao ikiwa programu ya MMMAM iliyozinduliwa rasmi kwenye halmashauri hizo mwezi Februari mwaka huu na kila halmashauri ilijivunia kuanza kutoa chakula shuleni ,upatikanaji wa chanjo kwa watoto,Mahudhurio ya kliniki kwa wajawazito na uanzishwaji wa madarasa ya Awali na Kwanza.


Mwenyekiti wa baraza la wazee Manispaa ya Shinyanga amesema Jigongwa Dittu katika tathimini hiyo ameona kuna upungufu wa maafisa ustawi na ufinyu wa bajeti ambao ni moyo wa utekelezaji wa Programu hiyo aliomba ifanyiwe kazi ili utekelezaji ufanyike kwa ufanisi mkubwa.


Mwakilishi kutoka Shirika la ICS mkoani Shinyanga Lucy Masanja ametoa ushauri kwa halmashauri kuwahusisha wadau wa sekta binafsi kwani wameonekana kuachwa washirikishwe lakini halmashauri Moja imeweza kuwaonyesha wadau hao wapewe elimu juu ya Programu ya MMMAM wataelewa na kushiriki kwa nao inawagusa.

Mwakilishi kutoka Mtandao wa Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto nchini (TECDEN ) Christopher Peter amewapongeza halmashauri zote kuanza kupiga hatua nakutoa ushauri wadau wote wanaoshiriki kwa namna moja suala la Maendeleo kwa watoto waonyeshwe ili kufahamu mchango wao.
Baadhi ya wadau akiwemo Meneja wa Mradi kutoka shirika la THPS kwa wilaya ya Shinyanga na Kishapu Temba Fideli amesema baadhi ya shule zimelima na kupata chakula lakini waangalie chakula hicho cha namna gani ili watoto wasipatwe na utapiamlo pia Mratibu kutoka shirika la SHDEPHA+ Gwalusano Katolila amesema wako tayari kushirikiana ili kuhakikisha watoto wanakuwa kwenye ukuaji timilifu



Wajumbe wa Programu ya PJT-MMMAM mkoa wa Shinyanga wakiendelea kusikiliza tathimini.


Wadau wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuzinduliwa kwa kikao cha tathimini.








Post a Comment

0 Comments