Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha noti bandia zenye thamani ya shilingi 420,000
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata siraha moja aina ya Browning Pistol ambayo ilitumika katika tukio la unyang"anyi huko halmashauri ya Msalala, noti Bandia 42 zenye thamani ya shilingi 420,000 mabomba 10 ya maji pamoja na pikipiki tano.
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Kennedy Mgeni akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga leo June 26,2024, amesema vitu hivyo vilikamatwa katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Mei 26,2024 hadi June 25,2024 kwa kushirikiana na jamii katika falsafa yake ya polisi jamii katika kukabiliana na vitendo mbalibali vya kihalifu, na wahalifu kupitia misako na doria.
Mgani amesema katika msako huo wamefanikiwa kukamata vitu mbalimbali vinavyotumika katika masuala ya ramli chonganishi mtambo mmoja wa kutengenezea pombe haramu ya moshi, Tv moja meza mbili kabati moja la kuwekea Tv, milango miwili na madirisha manne ya chuma.
Amesema jumla ya watuhumiwa 25 wanashikiliwa katika vituo mbalimbali vya polisi kuhusiana na tuhuma za kufanya uharifu huku wakisubiri kufikishwa mahakamani na wengine wakipewa dhamana.
"Katika kipindi hicho cha mwezi mmoja, jumla ya kesi nane zilihukumiwa mahakamani kwa mafanikio kama ifuatavyo, kesi mbili za kulawiti zilihukumiwa kifungo cha maisha jela, kesi moja ya kujeruhi ilihukumiwa kifungo cha miaka mitatu kesi mbili za wizi zilihukumiwa kulipa faini ya shilingi 300,000, kesi moja ya kupatikana na bangi ilihukumiwa kifungo cha nje miezi 12 na kesi moja ya kubaka ilihukumiwa kifungo cha nje miezi sita mtuhumiwa alikuwa na umri wa miaka 17"amesema Mgani.
Akieleza kwa upande wa usalama barabarani jumla ya makosa 3438 ya magari yalikamatwa, na makosa ya pikipiki na bajaji yalikuwa ni 1,496 huku dereva mmoja wa magari akifungiwa leseni yake kwa kukiuka sheria za usalama barabarani .
Aidha jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linatoa wito kwa wananchi wote kuendelea kuzingatia sheria za nchi, ili kuweza kushughulika na kazi zingine za ki uchumi ambazo ni halali kuliko kujiingiza kwenye kazi za kihalifu.
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha Noti bandia
Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga Kennedy Mgani akionyesha vifaa vya kufanyia uganga