*Amenyanyua kikokotoo, Ndejembi asema huo ni mwanzo tu
Nukuu za Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi- Bungeni
"Bajeti Kuu ya Serikali ya Mwaka wa fedha 2024/2025 ambayo tunaenda kuipitisha inaonyesha ni namna gani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anaguswa na maisha ya wafanyakazi wa nchi hii. Tangu aingie madarakani mwaka wake wa kwanza alipandisha madaraja yaliyokwama kwa miaka mingi, wafanyakazi waliokuwa hawajapandishwa maradaja kwa miaka Tisa (09), alipandisha zaidi ya watumishi 222,000" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Mheshimiwa Rais aliguswa sana na madeni kwa watumishi wa Umma, alitoa fedha kwaajili ya kulipa madeni hayo ya watumishi" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Julai 2022 kuna mabadiriko ya Kikokotoo yalifanyika, waliokuwa watumishi wa Umma walitoka kulipwa mkupuo wa Asilimia 50 na kushuka Asilimia 33. Waliokuwa Asilimia 25 walipanda kwenda Asilimia 33. Ilikuwa ni kilio kwa watumishi ambao mishahara yao ni ya chini na husubiria mkupuo wa fedha hizi kuanza maisha yao wanapokuwa wamestaafu" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Wizara ya Fedha mwaka wa fedha 2024/2025 wameweka Shilingi Bilioni 155 kwaajili ya kulipa Kikokotoo kunyanyua kutoka Asilimia 33 kwa waliokuwa Asilimia 50 kabla ya Julai 2022 kwenda Asilimia 40. Waliokuwa Asilimia 25 wamekwenda Asilimia 35" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Wabunge wengi mmezungumzia suala la kuangalia kiwango kiendelee kunyanyuka kurejea kilipokuwa Asilimia 50. Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri wameshukuru Asilimia 40 lakini wanaomba iweze kurudi Asilimia 50. Huu ni mwanzo mzuri ndiyo maana Asilimia 7 imewekwa" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi
"Serikali itazidi kuangalia ni namna gani itarudi katika Asilimia 50 ya Kikokotoo. Wanaoenda kulipwa siyo tu wanaokwenda kustaafu kuanzia 01 Julai, 2024. Wanaenda kulipwa wote hata wale waliostaafu kuanzia Julai 2022" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi.
"Watumishi 17,068 toka Julai 2022 wanaenda kulipwa mapunjo yao ya Asilimia 7 waliyostahili kupata. Waliokuwa wanapata Asilimia 33 kwenda Asilimia 35 watalipwa mapunjo yao ya Asilimia 2. Tunatarajia kuona wengi wakija kudai mapunjo ya mafao yao" - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Deogratius Ndejembi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464