Header Ads Widget

SHIRIKA LA TCRS LAKUTANA NA WADAU WA KILIMO, MIFUGO NA MASOKO KUJADILI MAFANIKIO YA MRADI



Wadau wa Kilimo, mifugo na masoko wa wilaya za Shinyanga na kishapu.

Na Frank Mshana, kishapu

TANGANYIKA Christian Refugee Service (TCRS) na wadau wa kilimo, mifugo na masoko Wilaya za Kishapu na Shinyanga wakiwemo wakulima na wafugaji wa vikundi vinavyowezeshwa na Shirika hilo wamekutana pamoja Kujadili Mafanikio ya mradi wa Usalama wa chakula na Kupunguza Njaa unaotekelezwa katika baadhi ya kata za Wilaya ya kishapu na Wilaya ya Shinyanga kwa ufadhili wa Norwegian Church Aid (NCA).

 

Msimamizi wa mradi wa TCRS Kishapu Dkt. Oscar Rutenge akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliowashirikisha watu mbalimbali wakiwemo madiwani,maofisa Lishe wa Wilaya, maofisa kilimo, mifugo na uvuvi wa wilaya, afisa maendeleo ya jamii wa wilaya kutoka  wilaya za Kishapu na Shinyanga. Mashirika mbalimbali  umma, likiwemo Shirika la uendelezaji wa viwanda vidogo SIDO, wasambazaji wa Teknolojia ya umwagiliaji KickStart international pamoja na wanufaika wa Mradi.

                         

 Rutenge amesema malengo ni kuwaleta  wadau pamoja na walengwa wa mradi huo kujadili mambo mbalimbali yatakayoweza kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo ya utekelezaji wa mradi.

Rutenge amefafanua kuwa mradi  wa NANSEN -Food Security and Reduction of Hunger(FSRH), unafadhiliwa na shirika la Kimataifa la Norwegian Church Aid (NCA) akieleza pia  mradi unatekelezwa kwa ushirikiano na wataalam wa ughani (extension staff) kutoka idara za kilimo, mifugo na uvuvi pamoja maendeleo ya jamii halmashauri za wilya za Kishapu na Shinyanga huku akishukuru  halmashauri za Kishapu na Shinyanga kutoa ushirikiano kwa TCRS katika  utekelezaji wake hali ambayo inahakikisha uendelevu wa wanufaika kupata huduma za ughani hata baada ya mradi kuisha muda wake. 

Ametaja baadhi ya mambo yaliyojadiliwa kuwa ni pamoja upatikanaji wa huduma za ughani, upatikanaji wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea, mbegu na viuatilifu, namna bora ya kuongezea thamani mazao ya bustani na upatikanaji wa masoko.       

Akiongelea suala la mikopo kwa wakulima wa bustani za mbogambioga na wafugaji wa wadogo wadogo  wakiwemo kuku  walioboreshwa  Afisa uendelezaji biashara wa SIDO kutoka  mkoani  Shinyanga bwana Joseph Tabani amesema kupitia changamoto ya mitaji, SIDO inatoa mikopo yenye riba nafuu kwa wajasiriamali  kuendeleza biashara zao ambapo amewataka wanufaika wa mradi wa Usalama wa chakula na Kupunguza njaa kutumia fursa hiyo na kuachana na mikopo umiza au kausha damu inayotolewa na watu wasio na taasisi rasmi  za fedhai.

                 

Nao wanufaika wa mradi huo wamesema waliupokea vizuri mradi huo na kwa sasa wanapata faida inayowawezesha kumudu kutunza familia zao kupitia kilimo mcha bustani za mboga mboga na ufugaji wa kuku chotara(walioboreshwa).

                                    

Samwel Maganga ni mdau wa kilimo kutoka shirika la usambazaji wa teknolojia ya umwagiliaji KickStart International amesema wakati umefika sasa kuachana na kilimo cha kutegemea mvua na kuwashauri wanufaika kuanza matumizi ya pampu rahisi zinazotumia  nguvu ya miguu katika kusukuma maji kumwagilia bustani zao hali itakayowakwamua kiuchumi. Sambamba na hilo amewaonyesha kwa vitendo sampuli za pampu za kumwagilia na jinsi zinavyotumika huku akieleza namna zinavyopatikana.

                            

Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni mwakilishi wa mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mheshimiwa Frednand Mpogomi amesema mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri itaanza kutoka mwezi Julai mwaka huu na kuwataka wanufaika wa mradi huo kuwa tayari kujiunga  katika vikundi vyao kuchangamkia fursa ya kuomba mikopo hiyo.


Afisa lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Saidi Mankiligo amekiri kuwepo kwa mafanikio chanya kwa wanufaika wa mradi huo wa usalama wa chakula na kupunguza njaa unaotekelezwa na Shirika la TCRS kwa ufadhili wa NCA.

Naye afisa Maendeleo ya jamii wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Happiness Isaeli akimwakilisha  mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya Jamii amesema katika Halmashauri ya Shinyanga TCRS imewezesha vikundi tisa vya kilimo cha bustani za mbogamboga na ufugaji wa kuku chotara ambapo vikundi vinne vimewezeshwa teknolojia rahisi ya umwagiliaji na kueleza kuwa kuna mafanikio makubwa. 

 kwa upande wa usalama wa chakula na kupunguza njaa pamoja na kujihifadhia kipato cha kuwezesha familia zao kipato ambacho kinawezesha wananchi kununua aina za vyakula wanavyotaka.  Aliongeza “Halmashauri inatamani teknolojia na fursa hiyo ifike kwa vijana na kinamama wa kata zote zinazounda halmashauri hiyo ikiwemo teknolojia ya umwagiliaji.”

                                 

Bw. Frank Lunyembeleka ambaye ni afisa mifugo na uvuvi kata ya Sekebugoro pia  mwezeshaji wa vikundi vya wakulima na wafugaji vinavyowezeshwa na TCRS, amesema kikao hicho ni muafaka wa kufikia malengo tarajiwa. Lengo la TCRS ni kuwafanya wanufaika kuweza kufanya shughuli za kilimo bora na ufugaji hata kama shIrika halipo na muitikio wa wakulima na wafugaji kujitiokeza kujiunga kwenye vikundi vinavyowezeshwa na TCRS umeongezeka hali ambayo inaonyesha kuna mafanikio chanya.

                        

Mheshimiwa Ngasa Mboje ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga amelitaka shirika la SIDO kuja na Teknolojia rahisi ya kuchakata mazao na kuyaongezea thamani kwakuwa wakulima wadogo na wafugaji hao uwezo wa kununua mitambo mikubwa hawana lengo likiwa ni kuwakwamua katika hali duni.

















Post a Comment

0 Comments