UKATILI WA WATOTO UTAONDOKA KAMA NGUZO TATU ZITAWAJIBIKA
Kwa kipindi cha
takribani zaidi ya miaka mitano baada ya kuanzishwa kwa Mpango Mkakati wa Taifa
wa Kutokomeza Vitendo vya Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwa
mkoa wa Shinyanga imeweza kupiga hatua kupunguza vitendo vya ukatili kwa
watoto.
Ili kuendelea kuviondoa
kabisa vitendo vya ukatili Wadau mkoani Shinyanga kupitia maadhimisho ya siku
ya Mtoto wa Afrika inayofanyika kila mwaka mwezi June,16 wameshauri viongozi wa
dini,familia,jamii na serikali kuungana kwa kusudio moja la kumkomboa mtoto.
Matukio mbalimbali ambayo
yamekuwa yakiwakuta watoto na kuwaathiri kisaikolojia katika mwenendo wa makuzi
yao ni ubakaji,ulawiti,mimba na ndoa za utotoni
,ajira kwa watoto,mauaji ukosefu wa mazingira salama ya utoaji elimu ikiwemo migogoro
ya familia.
Maadhimisho hayo yaliamabatana na kauli mbiu "Elimu jumuishi kwa watoto ,izingatie maarifa,maadili na stadi kazi.
Chombo cha habari za Shinyanga press club blog ,kilifanya uchambuzi juu ya ulinzi na usalama wa watoto kwa kutafuta maoni ya watu mbalimbali ili kuangazia hali ya utekelezaji wa MTAKUWWA ndani ya mkoa wa Shinyanga.
VIONGOZI WA DINI
Kauli za viongozi wa
dini mkoa wa Shinyanga Nuhu Manoni kutoka Jumuiya ya Kikrito (CCT) alibainisha
kuwa nyumba za ibada haziko kimya katika kukemea hali ya mifumo kandamizi ndani
ya jamii inayoathiri watoto na wanawake.
”Nyumba za ibada zina
idara za wanawake, watoto na vijana na tunatumia majukwaa hayo kutoa elimu ya
kutambua haki zao”anasema Manoni.
WADAU
WA KUPINGA VITENDO VYA UKATILI
John Eddy kutoka shirika la WEADOA anasema familia ndiyo taasisi ya kwanza katika kusimamia hali ya maadili na mmomonyoko wa maadili kabla ya serikali na jumba za ibada kuelekeza maadili.
Cecilia Msangwa kutoka shirika la YAWE anasema Mila ya Shikome iliyokuwa inatumiwa na
wasukuma inatakiwa kurejshwa ili kuweza
kuwapa wanafamila nafasi ya kujadili hali ya maadili katika familia na jamii.
“ Naona mila ya shikome
inapaswa kurejea ili kuwapa wazazi nafasi ya kuwaonya na kujadili kuhus maadili
kwa hali ya sasa,maana wazazi na walezi wamekuwa wakitumia muda mwingi kwenye utafutaji na kushidwa kujadiliana na watoto wao kwa kuwaweka kwenye uwazi wa vitendo visivyofa na vinavyofaa”anasema
Msangwa.
John Shija kutoka kituo
cha Msaada wa sheria mkoani Shinyanga (PACESHI) Sheria na kanuni za kusimamia
ulinzi na usalama wa watoto zimeainishwa kwaajili ya kuonyesha adhabu na hukumu
kwa watu wanaotenda ukatili dhidi ya watoto.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza
la watoto mkoa wa Shinyanga Noelina
Nicolaus akizungumza kwenye maadhimisho
ya siku ya Mtoto wa Afrika
amewataka wazazi kuacha
kuwafanyia ukatili watoto na kuwatimizia mahitaji yao yote wakiwemo watoto
wenye ulemavu kutowabagua.
Nicolaus amewasihi
wazazi pia kuendeleza vipaji vya watoto
wao ili wapate ujuzi na hata wanapofikia hatua ya utu uzima wapate kujiajiri
wenyewe.
Ametoa wito kwa watoto wenzao wawe na maadili mema na kuwasikiliza wazazi wao pia kutojiingiza kwenye makundi mabaya na kusababisha mmomonyoko wa maadili.
Naye, Helly Peter alikemea na kulaani tukio la kuawa kwa mtoto mwenye ualibino huko mkoani kagera,Asimwe Novart(2)
"Aliyeuwa haipaswi kwa kweli na tunapaswa kutoa elimu na tuendelea kutokomeza haya mambo mbaya,ukatili uliofanyika kwa mwenzetu haufai"anasema Peter.
JUHUDI
ZA MKOA
Mkoa wa Shinyanga
umeendelea kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake
na watoto kwa kutunga Mpango kazi wa mkoa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake
na watoto na kuungana ili kuwepo na mfano wa kuigwa.
Afisa Maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga,Rehema Edson ameitaka jamii,mashirika na viongozi wa dini na serikali kkungana kwa pamoja kupinga vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na kutekeleza mahitaji yao.
Naye, Mratibu wa Mtakuwwa,
Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Aisha Omary anakiri kunufaika katika juhudi
za kutomeza ukatili kwa Halmashauri hiyo.
“Sisi Halmashauri ya
wilaya ya Shinyanga ni wanufaika wakubwa wa Muungano huu wa wadau na
tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na
watoto”anasema Omary.
MFUKO WA WANAWAKE TANZANIA(WFT-T)
Baadhi ya mashirika ngazi ya Taifa wamefanikiwa kutoa ruzuku kwa asasi za kirai kwa ajili ya utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili mkoani Shinyanga.
Mratibu wa Shirika la Mfuko
wa wanawake Tanzania (WFT-T) mkoa wa
Shinyanga Gloria Mbia anasema wamefanikiwa kutoa ruzuku 40 kwa awamu tano kwa asasi 12 za kirai kwa
ajili ya utetezi wa haki za wanawake na watoto kwa Halmashauri ya wilaya ya
Shinyanga.
“Matokeo makubwa ni
hatua ya Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kutenga bajeti kwa masuala ya
ukatili kila mwaka”anasema Mbia.
OFISI YA MASHITAKA
“ili kurahisisha utoaji
wa haki, ofisi yetu ina mpango mkakati
wa kutoa gharama za nauli na malazi kwa shaidi anayetoka nje ya manispaa
ya Shinyanga.
WAZEE
WA MILA
Vilevile viongozi wamila na desturi walilamikia kutoweka mila ya Shikome iliyoku ikitumiwa kama sehemu ya kujenga maadili mema kwa watoto. Mwenyekiti wa machafu mkoa wa Shinyanga Njange kidola anasema” zamani kulikuwa na shikome lakini sasa hivi wazazi na wakuwa bise na wakiridu majumbani usku muda wa kukaa na watoto haminani wakati wa jamii kujitafakari kufanya mabadiliko”
NGUVU
YA TAPO
Mwakilishi kutoka TAPO la SHYEVAWC Musa Ngangala anasema Juhudi zingine za mafanikio ni kuimarisha usalama na ulinzi wa watoto kupitia Umoja wa kikundi kazi cha asasi za kirai zipatazo 30 zinazotekeleza afua za kutokomeza ukatili mkoa wa Shinyanga
Umoja wa
kikundi kazi hicho ambapo umetekeleza
jukumu kwa kuzingatia maeneo manne ikiwa ni uratibu, uzuaji, utoaji wa huduma
kwa wahanga wa ukatili na upelekaji wa habari na mawasiliano wa jamii.
“Ni vyema kwenda mbali nakuungana na wenzako ili kufikia malengo na nia yetu ni kuona haki
inapatikana kwa wanawake na watoto”anasema
Ngangala.
VYOMBO VYA HABARI
Mwandishi wa habari
mkoani Shinyanga Kareny Masasy anaeleza mchango wa vyombo vya habari
ulivyoweza kuibua na kuleta mafanikio kwa kuripotiwa matukio mengi.
Kwa mujibu wa
taarifa kutoka wizara ya afya umeonyesha
mkoa wa Shinyanga umekuwa nafasi ya pili
katika kuripoti masuala ya ukatili wa
kijinsia na watoto ikiwa matukio 12,300 yaliripotiwa.
“Waandishi tumepaza sauti zetu kwenye vyombo vya
habari kupitia mradi wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kufikia
mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla”anasema Masasy
JESHI LA POLISI
Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi,akizungumza wakati wa kampeni ya ONGEA NAO ,aliwahi kusema,matendo ya ukatili wa kijinsia ni pamoja na ubakaji, ulawiti vipigo, kutelekeza familia, kutumikisha watoto na kuwazorotesha masomo, lugha za matusi na ndoa za utotoni huku akiyataja madhara ya ukatili wa kijinsia kuwa ni pamoja na vifo, mimba za utotoni, maradhi yanayosababishwa na ngono mfano UKIMWI, ulemavu wa kudumu, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, umaskini, msongo wa mawazo, na migogoro ya kifamilia."Jeshi la Polisi tunawataka wanafunzi, wananchi ,wadau kutambua kuwa mnawajibu wa kupaza sauti na kutoa taarifa za uhalifu katika vyombo vya sheria ili kukomesha vitendo hivyo katika jamii inayozunguuka, kwani jukumu la ulinzi na usalama ni la kila mwananchi",amesema Kamanda Magomi
"Pia mnapaswa kutambua mifumo mbalimbali ya utoaji taarifa za ukatili wa kijinsi ambayo ipo katika jamii zetu. Mifumo hiyo ni pamoja na viongozi wa dini, dawati la jinsia polisi, ustawi wa jamii, viongozi wa serikali za mitaa au mtu yeyote anaaminika anaweza kutoa msaada. Hivyo basi niwaombe au nitoe rai kwa wananchi wote wa mkoa wa Shinyanga tuungane kwa pamoja mkoa wetu uendelee kuwa salama" Amesema Magomi
CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Shinyanga Rehema Namanilo
amesema takwimu za kufanyiwa ukatili zinatisha ni vizuri jeshi la polisi
likatenda haki likasimamia ipasavyo angalau likawabana wahalifu wakapewa adhabu
yao na litoe elimu kuanzia ngazi ya vitongoji ili watu hao waliokandokando ya
mji wawe na uelewa wa kutoa ushahidi.
MWISHO.