Wananchi wa Kijiji cha Nzoza kata ya salawe Wilayani Shinyanga wamelalamikia barabara waliyoijenga kwa nguvu zao wenyewe kwa lengo la kuunganisha kijiji chao na maeneo ya huduma za kijamii kutelekezwa na serikali bila kuwekwa makalavati wakidai kuwa hali hiyo inasababisha wanawake wajawazito kujifungulia njiani na wanafunzi wakike kufanyiwa vitendo vya ukatili wakijinsia kwa kuchelewa njiani wakati wa kwenda na kurudi shule.
Wananchi wa Kijiji cha Nzoza wameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari wanaotekeleza mradi wa kupambana na kuzuia ukatili wakijinsia kwa wanawake na watoto unaofadhiliwa na shirika lisilo lakiserikali la Women Fund Tanzania (WFT) walipofika katika Kata ya salawe huku wananchi hao wakidai kuwa wamelazimika kufungua barabara hiyo ili kuondokana na changamoto nyingi ikiwemo utoro wa wanafunzi wakike wanaoacha masomo kwa kuadhibiwa wanapochelewa shule, wanawake wajawazito kujifungulia njiani na wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao kutoka mashambani.
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Nzoza bwana Zebedayo Charles amekiri kuwepo kwa changamoto nyingi zinazowakabili wananchi dhidi barabara hiyo na kueleza kuiwa nguvukazi ya wananchi iliyotumika kujenga barabara hiyio ni sawa na shilingi milioni 9.9.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya shule ya Sekondari Salawe Bwana. Masalu Lufyega amekiri kuwa baadahi ya wanafunzi wamekuwa wakishindwa kuhudhuria masomo kwa kutokana na barabara hiyo kutopitika kipindi cha mvua na akieleza kuwa idadi kubwa ya wanafunzi wakike ndio wanaokatisha masomo na kujikuta wanatumbukia kwenye wimbi la mimba za utotoni.
Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ya salawe Mheshimiwa Joseph Buyugu kwa niaba ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga amekiri kutambua changamoto hiyo na kueleza kuwa malalamiko ya wananchi ameshayafikisha kwenye bBaraza la Madiwani kwa ajili ya kutengewa bajeti ya kuweka makalavati na ukarabati kwenye maeneo korofi ya barabara hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Nzoza Kata ya Salawe wakipita kwa Shida kwenye dimbwi la maji lililoko kwenye barabara hiyo.