WANAWAKE WA KATA YA SALAWE WILAYANI SHINYANGA WAMELALAMIKIA WANAUME WANAOCHUKUA MAGUNIA YA MPUNGA MAJUMBANI NA KWENDA KUBADILISHANA NA NGONO KWA MAKAHABA.

WANAWAKE WA KATA YA SALAWE SHINYANGA WAKIVUNA MPUNGA MASHAMBANI.

πŸ”ΊπŸ”»★★★★★★★★πŸ”»πŸ”Ί

 Wanawake wa Kata ya Salawe Wilayani Shinyanga wamelalamikia tabia ya wanaume kwenye familia zao kuchukua magunia ya mpunga majumbani na kwenda kubadilishana na biashara ya ngono na wanawake makahaba maarufu kama nzige ambao wamevamia maeneo ya vijijini wakati huu wa mavuno.

hata hivyo wanawake hao wameeleza kuwa tabia hiyo imeibuka zaidi wakati huu wa mavuno ya zao la mpunga baada ya makundi ya makahaba hao maarufu kama nzige kufika katika maeneo ya miji midogo na kukodi vyumba kwenye nyumba za kulala wageni wakijidai kuwa ni wauza baa huku wakiwalaghai wanaume kuwaletea mazao kwa kubadilishana na ngono.

Bi.Odeta Mshumbus ni Afisa Kilimo Kata ya SDalawe amewianisha vitendo hivyo na ukatili wakijinsia kwakuwa vinasababisha familia nyingi kukosa chakula muda mfupi baada ya mavuno sambamba na wanawake na watoto wakike kufanyiwa vitendo vya ukatili wakijinsia kwa kurubuniwa baada ya njaa kuingia katika familia zao.

Mtendaji wa Kata ya salawe Bwana George Kuchibanda amethibitisha kuwepo kwa madada poa waliovamia kata hiyo kipindi hiki cha mavuno huku Afisa maendeleo ya jamii wa Kata hiyo Bi. Emmy Kwayu akidai kuwa elimu inaendelea kutolewa kwa njia ya mikutano ya hadhara kudhibitio hali hiyo.

Emmy Kwayu ni Afisa Maendeleo wa Kata ya Salawe Wilayani Shi nyanga ameeleza kuwa tabia ya wanaume wa eneo hilo kuuza mazao bila kuishirikisha familia inasababishwa na mila na desturi potofu ambazo zimewaathiri wanawake kushindwa kujieleza na kusababisha wakibakia kuumizwa na ukatili wa kiuchumi wanaofanyiwa na wanaume wao.

Kwaupande wake mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bwana. Anamringi Macha ameziagiza halmashauri zote zinazounda mkoa huo kufuatilia ujuio wa Makahaba wanaobadilishana mazao na ngono sambamba na wanunuzi wasio rasmi wanaofika mashambani kununua mazao kwa vipimo vya rumbesa.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Anamringi Macha akitoa kauli ya Serukali kudhibiti wimbi la Madada Poa wanaobadilishana mazao na Biashara ya Ngono Mkoani Humo.

Baadhi ya wakulima Wakikusanya Mpunga waliovuna Mashambani.

          Kazi ya kuvuna Mpunga  Ikiendelea Shambani

                                 Kazi ya kuvuna Mpunga Ikiendelea Shambani

Mpunga ulioiva Shambani tayari kwa kuvunwa.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464