Header Ads Widget

TYC WAZINDUA KITUO CHA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KUPITIA UZALISHAJI SABUNI ZA MAJI''JAMII SOAP"

TYC WAZINDUA KITUO CHA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KUPITIA UZALISHAJI SABUNI ZA MAJI''JAMII SOAP"

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
SHIRIKA la Tanzanian Youth and Children (TYC) limezindua Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji “Jamii Soap”

Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 2,2024 na Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois, akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Juius Mtatiro, na kuhudhuliwa na wanawake Wajasiriamali, wakiwamo wale ambao awali walishapewa Mafunzo ya uzalishaji Sabuni na Shirika hilo la TYC.
Mkurugenzi wa Shirika la TYC Lucas Daudi, amesema Shirika hilo wapo kweye utekeleza Mradi wa kuwawezesha Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni, kwa ufadhili wa Tanzania Development Trust, ndiyo maana wanawajengea wanawake ujuzi wa kuzalisha Sabuni za Maji ili wapate kipato na kuondokana na Adui Maskini.

Amesema kabla ya kutekeleza Mradi huo walifanya utafiti na kugundua kwamba asilimia 87 ya Sabuni hapa nchini zinatoka Nje ya Nchi, lakini Malighafi za utengenezaji wa Sabuni hizo zinatoka hapa hapa Tanzania.
“Baada ya kufanya utafiti na kugundua pia Tanzania kuna uhitaji mkubwa wa Sabuni, ndipo tukaja na Mradi wa kuwajengea Wanawake ujuzi wa uzalishaji Sabuni ili watumie fursa hiyo kujikwamua kiuchumi.”amesema Daudi.

“Mradi huu umejikitika kabisa kwa Wanawake sababu ndiyo waathirika wakubwa wa uchumi na wana mahitaji mengi, hivyo wakijikwamua kiuchumi hata vitendo vya ukatili vitapungua, sababu chimbuko la ukatili ni umaskini,”ameongeza.
Mjumbe wa Bodi wa TYC Ntimba Daniel,amesema kupitia Kituo hicho pia wanawake watajengewa uwezo wa kuendesha Biashara zao pamoja na mbinu za kupata Masoko, na kitatoa fursa ya Ajira kwa vijana.

Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akimwakilisha Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro, amelipongeza Shirika hilo kwa kumkomboa mwanamke kiuchumi,na kwamba mwanamke akiwezeshwa ni ukombozi kwa familia na Taifa kwa ujumla.
“Ukiwekeza kwa Mwanamke hutopoteza kitu chochote, hivyo Shirika hili nalipongeza sana na Serikali ipo pamoja na nyie, kwa kuhakikisha Mwanamke anakombolewa kiuchumi,”amesema Telezia.

Aidha, ametumia pia fursa hiyo kutoa wito kwa wanawake Wajasiriamali, kwamba wasije wakajiingiza kwenye mikopo kausha damu, bali watumie fursa ya Mikopo ya Halmashauri Asilimia 10 ambayo itaanza kutolewa hivi karibuni.
Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddy, ametoa wito kwa wanawake Wajasiriamali kuchangamkia fursa ya Mikopo ya Benki hiyo, kupitia Programu ya Imbeju ambayo inatolewa kwa Mjasiriamali Mmoja Mmoja ambaye amejiunga kwenye kikundi, na kwamba haina Riba na huanza kutolewa kuanzia Sh. Laki 2 hadi Milioni 10.

Mmoja wa wanawake Wajasiriamali ambaye amenufaika na Mafunzo ya utengenezaji wa Sabuni kutoka TYC Elizabeth William, ameshukuru kujengewa uwezo wa kuzalisha Sabuni na sasa yupo vizuri kiuchumi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji.
Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji.
Mkurugenzi wa Shirika la TYC Lucas Daudi akielezea uzinduzi huo wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji Sabuni za Maji.
Mkurugenzi wa Shirika la TYC Lucas Daudi akiendelea kuzungumza kwenye uzinduzi huo wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji Sabuni za Maji.
Mjumbe wa Bodi wa TYC Ntimba Daniel akisoma Risala kwenye hafla hiyo.
Afisa Mawasiliano wa Shirika la TYC Aloyce Mikomangwa akisherehesha hafla hiyo.
Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddy, akizungumza kwenye hafla hiyo.
Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddy, akiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo.
Meneja Biashara kutoka Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mwanahamisi Iddy, akiendelea kuzungumza kwenye Hafla hiyo.
Wadau wakiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau wakiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo.
Wadau wakiendelea kuzungumza kwenye hafla hiyo.
Mjasiriamali Elizabeth Wiliam akielezea namna alivyonufaika na Mafunzo ya uzalishaji wa Sabuni za Maji kupitia Shirika la TYC.
Mjasiriamali Grace Biteke akielezea namna alivyonufaika na Mafunzo ya uzalishaji wa Sabuni za Maji kupitia Shirika la TYC.
Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akiwa kwenye hafla hiyo akifuatilia kwa makini tukio zima.
Wajasiriamali wakiwa kwenye hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji kutoka TYC.
Hafla ikiendelea ya uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji.
Hafla ikiendelea ya uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji.
Hafla ikiendelea ya Uzinduzi wa Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji wa Sabuni za Maji.

Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akikata Utepe kuzindua Kituo cha Uwezeshaji Wanawake kiuchumi kupitia uzalishaji Sabuni za Maji kutoka Shirika la TYC.

Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akiangalia bidhaa za Sabuni za Maji ambazo tayari zimezalishwa na Wajawasiriamali waliojengewa uwezo na Shirika la TYC.
Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois akiangalia bidhaa za Sabuni za Maji ambazo tayari zimezalishwa na Wajawasiriamali waliojengewa uwezo na Shirika la TYC.
Mgeni Rasmi Afisa Tarafa ya Shinyanga Mjini Telezia Alois (wapili kutoka kulia )akiangalia bidhaa za Sabuni za Maji ambazo tayari zimezalishwa na Wajawasiriamali waliojengewa uwezo na Shirika la TYC.
Meneja Biashara Benki ya CRDB Tawi la Shinyanga Mjini Mwanahamisi Iddy akiangalia bidhaa za Sabuni za Maji, "Jamii Soap" ambazo tayari zimezalishwa na Wajawasiriamali waliojengewa uwezo na Shirika la TYC.
Picha ya pamoja ikipigwa.

Post a Comment

0 Comments