CHIFU KUTOKA KENYA KABILA LA WAKAMBA AZINDUA RASMI TAMASHA LA UTAMADUNI SANJO YA BUSIYA NEGEZI WILAYANI KISHAPU

TAMASHA LA SANJO YA BUSIYA -77FEST LAZINDULIWA RASM

xxx

Chifu Kutoka Nchini KENYA wa Kaunti ya kitui Kwa kabila la wakamba Dr Augustus Muli amezindua Tamasha la Utamaduni la SANJO YA BUSIYA-77FEST Mkoani Shinyanga..


Chifu Muli amezindua Tamasha Hilo Kwa kupiga Ngoma za milango ambazo ni Ngoma maalumu Kwaajili Chifu pekee

Tukio la uzinduzi limehudhuriwa na Chief wa Utemi wa Busiya Ntemi Edward makwaia Pamoja na Machifu wengine kutoka Jijini Mwanza .

Kilele Cha Tamasha la SANJO YA BUSIYA -77FEST kinatarajiwa Kuwa jumapili hii kwenye viwanja vya ikulu ya Negeji -Kishapu Shinyanga huku maelfu ya watu wakitarajiwa kuhudhuria Tamasha hili ambalo hufikisha watu Elfu 40 Hadi 50 kutoka maeneo mbalimbali Nchini.

LICHA ya Kuwa na burudani nyingi za Ngoma za kabila la wasukuma, Sanjo ya Busiya ya 2024 itanogeshwa na kikundi Cha Ngoma Cha Itumani kutoka kitui Kenya ambao wameongozana na chifu Muli
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464