WAZEE SHINYANGA WANA IMANI NA KATAMBI

WAZEE SHINYANGA WANA IMANI NA KATAMBI

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
BARAZA la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga,wameeleza kuwa na imani na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,kutokana na utendaji wake kazi wa kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo pamoja na kutatua matatizo ya wazee.

Wamebainisha hayo leo Julai 13,2024 wakati Mbunge Katambi alipofanya Mkutano na Wazee wa Manispaa ya Shinyanga,kuchota busara zao ili aendelee kuwa kiongozi bora.
Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano, akisoma andiko la wazee wamempongeza Mbunge Katambi namna wanavyochapa kazi ya kuwatumia wananchi na kuwaletea maendeleo,na kwamba ndani ya miaka Minne ya Ubunge wake,Shinyanga imekuwa na maendeleo makubwa.

"Tunakupongeza Mbunge wetu Katambi kwa kazi kubwa ambayo unaifanya hapa Shinyanga,pamoja na Serikali kwa ujumla chini ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan, kwa kutujali pia wazee na hata kuunda mabaraza ya ushauri ya wazee kuanzia ngazi za chini kabisa na kushughulikia matatizo yetu,"amesema Tano.
Aidha,wazee hao kupitia andiko lao wameiomba Serikali kusaidia kuinua ustawi wa maisha ya wazee,ulinzi, kupata huduma bora za matibabu yakiwamo madawa ya wazee na vitambulisho vya matibabu bure.

"Wazee tunakabiliwa na magonjwa yasiyo ya kuambukiza,na magonjwa haya yanatuua sana,tunaomba Serikali iboreshe huduma na kutupatia matibabu bure, sababu wazee hawana fedha za kulipia gharama za matibabu,"amesema Tano.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Benard Itendele,amemtaka Mbunge Katambi kwamba aendelee kuchapa kazi na asiteteleke kutokana na maneno ya wakosaji, na kwamba mti wenye matunda ndiyo unaopigwa mawe.

"Ukiwa kiongozi ni jalala,maneno ya wakosaji hayakosekani hasa kwa kiongozi mchapakazi kama wewe, nawaomba wazee tumuunge mkono kijana wetu Katambi,"amesema Itendele.
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha,amewaambia wazee hao kwamba wana Mbunge mchapakazi na mwenye nidhamu, sababu anathamini watu wa rika lote na leo amekutana na wazee.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Anorld Makombe,amewaomba wazee hao kwamba wasisite pia kufika kwenye Ofisi za CCM kutoa ushauri,na kwamba watawatumia pi kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa,ili kupata wagombea wazuri na wenye sifa.
Katambi akizungumza kwenye kikao hicho,amesema amekutana na wazee hao ili kuchota busara zao,sababu wazee ndiyo dira ya nchi,na kwamba kiongozi yoyote atakae dharau wazee hawezi kuwa kiongozi bora na taifa litaangamia.

"Wazee ndiyo waliolifikisha taifa letu hapa,na leo nchi ina amani na utulivu na sisi tumekuwa viongozi sababu ya nyie wazee, na hata Rais wetu Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan anawapenda sana, na changamoto zenu zote zitaendelea kutatuliwa,"amesema Katambi.
Amewaomba pia wazee kulipigia kelele na kulikemea tatizo la Mmomonyoko wa maadili,ambalo limekuwa tatizo duniani kote ambalo linakwenda kupoteza taifa na hata kuja kukosa viongozi bora.

Ametumia pia fursa hiyo kuwaomba wazazi,kuacha malezi ya kisasa kwa watoto,ambayo ndiyo yamekuwa moja ya tatizo la Mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
Amewatoa hofu wazee hao kwamba Serikali chini ya Rais Samia,wataendelea kuboresha huduma za matibabu, na kwamba katika Manispaa ya Shinyanga zimetolewa fedha nyingi ikiwamo ujenzi wa hospitali na ununuzi wa vifaa tiba na madawa ya magonjwa ya wazee.

Katambi pia amewaeleza wazee hao miradi ya Maendeleo ambayo ameitekeleza kwa kipindi chake cha Ubunge ndani ya miaka Minne,kwamba ahadi zake alizoziahidi nyingi ametekeleza.
Katika Mkutano huo wazee pia walipewa kila Mmoja jiko la gesi kwa ajili ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Aidha,kwenye Mkutano huo wazee walikuwa wakiimba nyimbo za kuwa na imani na Mbunge Katambi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu akizungumza na Wazee wa Manispaa ya Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu akizungumza na Wazee wa Manispaa ya Shinyanga.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Anold Makombe akizungumza kwenye Mkutano huo.
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Hamisa Chacha akizungumza kwenye Mkutano huo.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye Mkutano huo.
Mwenyekiti wa Baraza la ushauri la wazee Manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akizungumza kwenye Mkutano huo.

Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Benard Itendele akizungumza kwenye Mkutano huo.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Wazee wakiwa kwenye Mkutano wao na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi,vijana, ajira na watu wenye ulemavu.
Picha ya pamoja ikipigwa.
Picha ya pamoja ikiendelea kupigwa.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464