KAMATI KUIPANDISHA TIMU YA STAND UNITED YA SHINYANGA KUSHIRIKI KUCHEZA LIGI KUU YA TANZANIA BARA HADHARANI
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro ambaye ni mlezi wa timu ya stand united,ametangaza rasmi kamati mbalimbali ambazo zitatekeleza majukumu ya kuipandisha timu hiyo kushiriki kucheza ligi kuu ya Tanzania bara.
Kamati hizo zimetangazwa leo julai 14,2024 kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (SHYCOM) na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa Michezo pamoja na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu.
Mbunge Katambi akizungumza kwenye kikao hicho.
Mtatiro kabla ya kuanza kutangaza kamati hizo ameishukuru Kampuni ya Jambo Food Product kwa kuipambania Timu hiyo ya Stand United kwa kuendelea kuifadhili hadi sasa ikiwa ina cheza ligi ya Championship.
"Leo tumekutana hapa kupeana mrejesho juu ya kikao kilichopita kwa kutangaza kamati mbalimbali ambazo zimeundwa ili kuendeleza timu yetu na kuipandisha kushiriki kucheza ligi kuu ya Tanzania bara,"amesema Mtatiro.
Ametangaza kamati hizo kuwa Kamati ya fedha itakuwa na Mkuu wa wilaya Julius Mtatiro, Seleman Hamis,Dk.Kalekwa Kasanga,Alexius Kagunze,Masudi Kibetu,Gasper Kileo,Patrobas Katambi, Ahmed Salum,Lucy Mayenga,Emmanuel Cherehani,Salome Makamba,Kija Makindo.
Wengine ni Geogre Shujaa,Gilitu Makula,Ally Amour, Masalu Lusana na Khadija Kabojela.
Mbunge Katambi akikabidhi Shilingi Milioni Moja kwa Timu ya Stand United.
Ametaja Kamati ya Usajili na Mashindano kwamba itakuwa na Musa Lyoba,Dk Hellyson Maeja,Sudi Juma,Juma Marwa,Jerry Julius,Chrispin Kakwaya,Stivian Antindius na Afande Tegemea.
Kamati ya Hamasa
Itakuwa na Bihemo Thomas,Anord Rwekiza, Omary Malula,Madam Sitta,Issa Mbaraka,Zaituni Kiboga,na Sadi Bonge.
Kamati ya Ulinzi.
Base Sunzu, Sadi Bonge,Sterwart Mathias,Fred Masai,Sospeter Kisobilo, na Peter Toshi.
Kamati ya Chakula.
Grace Joliga,Base Sunzu na Mbezi Kwilasa.
Kamati ya nidhamu na maadili.
Mzee Tendele,Wakili Kabudi,Mzee Gwama,Mzee Kazembe,na mtu mmoja kutoka Serikalini.
Kamati ya mapokezi.
Hamduni Khalfan,Michael Kaijage,Mseti Matiko,Sudi Juma,Mussa Lyoba,Chrispin Kakwaya na Stivian Antidius.
Kamati ya ufundi.
Steward Mathias,Msafiri Patric na Ngassa Swaganya.
Kamati ya manunuzi
Telezia Alois,Diana Msuya na mtu mmoja kutoka Serikalini.
Aidha,amewaomba wanachama wa Timu ya Stand United wajipange ili wawe na kadi za chama, na kwamba wana matarajio pia ya kufungua duka la kuuza bidhaa mbalimbali ambazo zitakuwa na nembo ya Stand United.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu,amesema kwa sasa timu ya stand united imepata viongozi makini na lazima itapanda kushiriki kucheza ligi kuu.
Ameziomba Kamati hizo kwamba zifanye kazi yao ipasavyo na mtu ambaye ataonekana kutaka kukwamisha jambo lolote wamsimamishe,huku akitoa ushauri kwa kamati ya usajili kwamba wasisahau kusajili wazawa.
Amesema Mkoa wa Shinyanga ukiwa na Timu ambayo inashiriki kucheza ligi kuu hata uchumi wake utaongezeka,huku akitoa kiasi cha Sh.milioni Moja,mipira Miwili na Set mbili za Jezi kwa timu ya Stand United kwa ajili ya kuanza kuwaunga mkono.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464