TARURA WAANZA MAANDALIZI UJENZI DARAJA LA MAWE LINALO UNGANISHA CHIBE NA OLDSHINYANGA

TARURA waanza maandalizi ujenzi daraja la mawe linalo unganisha Chibe na Oldshinyanga

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
WAKALA wa Barabara Mjini na Vijijini (TARURA)Mkoa wa Shinyanga,wameanza maandalizi ya ujenzi wa daraja la mawe ambalo linaunganisha Kata ya Chibe na Oldshinyanga,pamoja na kunufaisha pia wakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga.

Meneja wa (TARURA)Mkoa wa Shinyanga Mhandisi Avith Theodory,amesema daraja hilo litakuwa na urefu wa Mita 45 na gharama zake ni zaidi ya Milioni 120,ambalo litaimarisha mawasiliano na kuchochea uchumi kwa wananchi.

Awali Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro alifanya ziara kukagua ujenzi wa daraja hilo na kutoa maagizo ujenzi wake uharakishwe ili wananchi wapate huduma.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464