Header Ads Widget

MAHAKAMA MBILI ZA MWANZO MKOANI SHINYANGA KUVUNJWA NA KUJENGWA ZA KISASA

MAHAKAMA MBILI ZA MWANZO MKOANI SHINYANGA KUVUNJWA NA KUJENGWA ZA KISASA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MAHAKAMA ya Mwanzo iliyopo jirani na soko la nguzo nane Manispaa ya Shinyanga, pamoja na Mahakama ya mwanzo Manispaa ya Kahama zitavunjwa na kujengwa majengo mapya ya kisasa,pamoja na kuwekewa mfumo wa teknolojia ya Tehama.

Ujenzi wa Mahakama hizo mbili za Mwanzo Manispaa ya Shinyanga na Kahama mkoani Shinyanga,miongoni mwa Mahakama tatu za mwanzo,ambazo zinafanyiwa ujenzi wa kisasa ikiwamo Mahakama ya mwanzo mkoani Geita.
Hayo yamebainishwa leo Julai 28,2024 kwenye zoezi la makabidhiano ya eneo ilipo Mahakama hiyo ya mwanzo Manispaa ya Shinyanga,baina ya Mahakimu na Mkandarasi ambaye anatekeleza ujenzi huo kutoka Kampuni ya Parik Limited.

Mhandisi wa ujenzi kutoka makao makuu ya Mahakama ya Tanzania Fabian Michael, amesema mradi huo wa ujenzi wa majengo matatu ya kisasa katika Mahakama za mwanzo Manispaa ya Shinyanga, Kahama na Geita, utagharimu kiasi cha Sh,bilioni 3.6, na kwamba majengo ya awali yatavunjwa.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Frank Mahimbali, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa Mahakama mbili za mwanzo mkoani humo ya Shinyanga na Kahama kuhakikisha anakamilisha ujenzi huo ndani ya muda wa mkataba.

Naye Mkandarasi wa ujenzi ambaye anatekeleza mradi wa ujenzi huo kutoka kampuni ya Parik Ltd ya jijini Arusha Amon Germin, amesema atahakikisha anakamilisha ujenzi huo ndani ya miezi sita kulingana na mkataba wake.

Post a Comment

0 Comments