DAWA ZA KULEVYA... Orodha wauzaji o tayari, kazi inaanza
SERIKALI imesema imekamilisha kanzidata ya wauzaji wakubwa wa dawa za kulevya na imeanza uchunguzi wa watu hao, huku Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ikisema kila siku inapokea waraibu 900 wanaotumia dawa za usaidizi wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya ‘methadone’.
Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam katika mkutano wa waandishi wa habari na Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, pamoja na Mkurugenzi wa MNH, Prof. Mohamed Janabi.
Pamoja na mambo mengine, mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa taarifa kuhusu kukamatwa kwa wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO NIPASHE.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464