KATAMBI AGAWA MAJIKO YA GESI KWA WAZEE SHINYANGA

KATAMBI AGAWA MAJIKO YA GESI KWA WAZEE SHINYANGA

Wamuombea baraka katika uongozi wake,wataka aendelee kuwa Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MBUNGE wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi,ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana,Ajira na watu wenye ulemavu, ametimiza ahadi yake ya kuwapatia majiko ya gesi wazee wa manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwa Mabalozi Wazuri wa Utunzaji wa Mazingira na kutumia Nishati safi ya kupikia.

Majiko hayo yamekabidhiwa leo Julai 20,2024 na Katibu wake Samweli Jackson kwenye Ofisi za CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Samweli akizungumza wakati wa kukabidhi majiko hayo, amesema Julai 13 mwaka huu, Mbunge Katambi alipokutana na wazee wa Shinyanga, pamoja na kuzungumza nao mambo mbalimbali ikiwamo kuchota baraka za wazee, aliwaahidi wazee hao pia atawapatia majiko ya gesi kwa ajili ya matumizi ya nishati safi ya kupikia,ahadi ambayo ameitekeleza leo.

“Mbunge Katambi anawapenda sana wazee, na leo ametekeleza ahadi yake ya kuwapatia majiko ya gesi,wazee 85 yenye thamani ya Sh.milioni 4.2, na tangu tuanze kugawa majiko haya tumeshafikisha kugawa majiko 1,780 kwa makundi mbalimbali,lengo likiwa ni kuunga mkono Kampeni ya Rais Samia Suluhu Hassan ya utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia,”amesema Samweli.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga Stephano Tano,amemshukuru Katambi kwa kuwajali wazee na hata kuwapatia majiko ya gesi, na kuahidi watakuwa mabalozi wazuri wa utunzaji wa mazingira,huku wakimuombea Mbunge huyo Baraka kwa mwenyezi mungu na kuendelea kuwa mbunge wao kwa awamu nyingine tena 2025.

Nao baadhi ya wazee akiwamo Magreth Maduhu, amesema majiko hayo ya gesi yatakuwa na faida kwao hasa kwa wanawake, sababu wanapotumia kuni macho yao hua mekundu, na kuanza kutuhumiwa kuwa ni wachawi, lakini sasa hivi wakitumia nishati safi ya kupikia watakuwa wazee wa kisasa na kutoathiriwa tena na moshi.
Mzee mwingine John Kashinje,amesema juzi aligombana na mkewake sababu ya kumzuia kukata mti kwa ajili ya kupata kuni za kupikia,lakini sasa hivi baada ya kupata jiko hilo la gesi ugomvi na mkewake hautakuwepo tena.

Aidha,Mbunge Katambi amekuwa ni kawaida yake ya kugawa majiko ya gesi jimboni mwake, ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, katika kampeni yake ya kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kutunza mazingira, na kuachana na kuni na mkaa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson akizungumza kwa niaba ya Mbunge Katambi wakati akikabidhi majiko ya gesi kwa wazee wa Shinyanga.
Mwenyekiti wa baraza la ushauri la wazee manispaa ya Shinyanga Stephano Tano akizungumza kwenye hafla ya kukabidhiwa majiko ya gesi.
Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi ikiendelea kwa wazee wa Shinyanga.
Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Samweli Jackson (kushoto)akigawa majiko ya gesi kwa wazee.
Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi ikiendelea.
Hafla ya kukabidhi majiko ya gesi ikiendelea.
Muonekano wa majiko ya gesi.
Wazee wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa majiko ya gesi kwa wazee.

Wazee wakiwa kwenye hafla ya kukabidhiwa majiko ya gesi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464