RC MACHA AWASIHI WATANZANIA KUWAENZI MASHUJAA KWA KUDUMISHA AMANI YA NCHI
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amewasihi Watanzani kuwa enzi mashujaa ambao walipigania taifa hili kupata uhuru,kwa kudumisha amani na upendo.
Macha amebainisha hayo leo Julai 25,2024 ikiwa ni siku ya kumbukumbu ya kuwa enzi mashujaa wanchi hii, ambao walilipigania taifa kupata uhuru kwa kutumia silaha za jadi, maadhimisho ambayo katika Mkoa wa Shinyanga yamefanyika katika mnara wa mashujaa mazingira ‘Center’ Manispaa ya Shinyanga, na kuweka mashada na silaha za jadi.
Amesema Mashujaa hao walipigania Uhuru wa Taifa hili tena wakitumia silaha za Jadi, na hivyo kuwasihi Watanzania kuendelea kuwaenzi Mashujaa hao kwa kudumisha amani ya nchi.
“Tuwa enzi mashujaa wetu ambao walilipigania taifa hili kupata uhuru, kwa kuendelea kudumisha Amani, na wale ambao bado wapo hai tuwapongeze na kuwaenzi pia kwa kazi kubwa ambayo waliifanya ya kujitoa kwao ili Tanzania iwe huru,”amesema Macha.
“Nawasihi Watanzania tuilinde amani hii ambayo tunayo tusije ichezea, ni heli tufofautiane kwa vitu vingine lakini siyo kuvuruga Amani, Amani ikitoweka kuirudisha ni kazi,” ameongeza.
Aidha, amewasihi pia Watanzania kuwapongeza Marais walioliongoza taifa hili, pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliogoza Taifa katika amani na utulivu, na wamuombee katika utendaji wake kazi wa kuwatumikia na kuwaletea maendeleo.
Naoa baadhi ya viongozi wa dini wakitoa maombi kwenye maadhimisho hayo ya siku ya mashujaa, waliliombea amani taifa, huku akiahidi kuendelea kuhubiri amani kwenye nyumba za Ibada.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇