MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUKOMESHA UTORO KWA WANAFUNZI
Msitahiki Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe, Elias Masumbuko amewataka madiwani wote wa Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kutokomeza utoro kwa wanafunzi kwa shule za Msingi na Sekondari.
Mhe, Masumbuko ameyasema hayo leo julai 29,2024 katika kikao cha kawaida cha madiwani robo ya nne ya mwaka 20223/2024 cha kuwasilisha taarifa za utendaji kazi katika kata zao, ambapo amesema katika Manispaa ya Shinyanga bado utoro kwa wanafunzi ni mkubwa ambapo kawataka madiwani kusaidiana na maafisa Elimu Msingi na Sekondari ili kupunguza na kutokomeza utoro.
"Watoto wengi hawaendi shule kwa sababu ya changamoto za kimaisha sasa niwaombe waheshimiwa Madiwani twendeni tukasaidizane na maafisa elimu Msingi na Sekondari, tufanyeni jitihada za dhati kuhakikisha tunasaidiaana kuondoa utoro kwa wanafunzi wetu". Amesema Mhe, Msitahiki Meya.
Katika hatua nyingine madiwahi hao wamesema wanakabiliwa na changamoto za uhaba wa watendaji wa vijiji na mitaa ambapo wameiomba serikali kuwasaidia ili kupata watumishi hao.
Akitoa ufafanuzi wa upungufu wa watumishi Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi Rasilimali watu Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa ya shinyanga kwa mwaka wa fedha 2024/2025 imepata kibali cha kuajiri watumishi 151 katika nafasi mbalimbali ikiwemo Watendaji wa Vijiji na Mitaa.
"Ni kweli tatizo upungufu wa watumishi hususani watendaji wa vijiji na mitaa kwa Halmashauri yetu ni mkubwa lakini serikali kwa kutambua hilo halmashauri yetu imepata kibali cha kuaajiri watummishi 151kwa mwaka huu wa fedha ambapo watendaji wa Mitaa kumi na tano (15) watunza kumbukumbu wanne (4) na madereva watani (5) ambapo itasaidia kupunnguza kwa kiasi fulni upungufu wa watendaji kwennye maeneo yetu". Amesema Mkuu wa Division ya Utawala na Usimamizi Rasilimali watu Pius Sayayi amesema Halmashauri ya manispaa ya Shinyanga. Mhe Pius Sayayi.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464