Header Ads Widget

DC MTATIRO AFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI SALAWE NA KUTOA MAAGIZO JUU YA UTATUZI WA KERO HIZO


DC MTATIRO AFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI SALAWE NA KUTOA MAAGIZO JUU YA UTATUZI WA KERO HIZO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amefanya Mkutano mkubwa wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi wa Kata ya Salawe wilayani humo, na kutoa maagizo juu ya utatuzi wa kero hizo,huku akipiga marufuku wananchi kuchangishwa michango hovyo bila kuidhinishwa na Mkuu wa Wilaya. 

Mkutano huo umefanyika jana julai 10,2024,kwenye uwanja wa stendi ya mabasi Salawe.
Mtatiro akizungumza kwenye Mkutano huo,amesema wao kama viongozi wameteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan,kuja kumsaidia kazi pamoja na kutatua kero za wananchi.

"Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ameniteuwa kuja hapa Shinyanga kuhudumia wananchi,ndiyo maana ninafanya ziara kuzungumza na wananchi kwenye mikutano ya hadhara ili kujua kero zao na kuzitatua,"amesema Mtatiro.
"Serikali ya Rais Samia ni Serikali ya wananchi, na baada ya Mwenge kipita hapa Shinyanga Mwezi Agost, tuna anza ziara tena ya Kata kwa Kata kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua,yani tunawafuata wananchi walipo na kuhamishia Ofisi kwenye maeneo yao," ameongeza.

Akijibu kero mbalimbali za wananchi wa Salawe ikiwamo ya miundombinu ya barabara,ukosefu wa umeme zikiwamo taasisi za Serikali, maboma ya zahanati,maji, mikopo ya asilimia 10, ujambazi, ukosefu matundu ya vyoo shuleni,kukithiri watoto kuliwa na Fisi, na kituo cha afya salawe kutofanya kazi, amesema kwamba kero hizo zitatatuliwa na ameshatoa maelekezo ya utekelezwaji wake.
Aidha,kupitia Mkutano huo amepiga Marufuku suala la wananchi kuchangishwa michango hovyo, na kwamba ni marufuku wananchi kuchangishwa fedha kama michango hiyo haijaidhinishwa na Mkuu wa Wilaya.

"Ni marufuku mwananchi kuchangishwa mchango wowote kabla sijaidhinisha mimi Mkuu wa Wilaya, na huo ndiyo utaratibu wa Serikali,"amesema Mtatiro.
Akizungumzia pia suala la Kituo cha Afya Salawe, amesema kwamba baada ya mwezi Mmoja huduma zitaanza kutolewa ambapo wanakamilisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD) pamoja na maabara, na baada ya hapo watakuwa wakikamilisha majengo mawili mawili.

Kwa upande wa kero ya majambazi, ameagiza kwamba kuimarishwe suala la ulinzi Shirikishi, na hadi kufikia julai 20 awe ameshapewa mpango kazi wa kuanzisha suala hilo,ili wananchi wa Salawe pamoja na wafanyabiashara waishi kwa amani na utulivu.
Nao baadhi ya wananchi wa Salawe pamoja na kuwasilisha kero zao kwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,wamempongeza Rais Samia kwa kutoa fedha nyingi za miradi ya maendeleo, huku wakionyesha kuchukizwa na watendaji ambao ni wazembe, wanaotumia kauli yake vibaya ya kazi iendelee, kwa kuendeleza matumbo yao.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akizungumza na wananchi wa Salawe wilayani Shinyanga kwenye mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Salawe Joseph Buyugu akizungumza kwenye Mkutano huo.
Viongozi wakiwa kwenye mkutano huo.
Wananchi wakiwasilisha kero zao kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro kwenye mkutano.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Wananchi wakiendelea kuwasilisha kero zao.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments