Header Ads Widget

RC MACHA AMEWASIHI WANANCHI SHINYANGA WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIMA AFYA ZAO BURE,KAMPENI YA AFYA CODE CLINIC KUTOKA KAMPUNI YA JAMBO GROUP

RC MACHA AMEWASIHI WANANCHI SHINYANGA WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIMA AFYA ZAO BURE, KAMPENI YA AFYA CODE CLINIC KUTOKA KAMPUNI YA JAMBO GROUP

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,amezindua Rasmi Kampeni ya utoaji matibabu bure kwa wananchi, huku akiwasihi wajitokeze kwa wingi kwenye kampeni hiyo ili kupata huduma za matibabu na kuimarisha afya zao.

Kampeni hiyo ya utoaji matibabu bure (afya code clinic) imeratibiwa na Kampuni ya Jambo Group Limited kwa kushirikiana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ikishikwa mkono pia na benki ya CRDB.
Macha akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, ameipongeza kampuni ya jambo kwa kushirikiana na Serikali kuandaa huduma hiyo, ambayo itaimarisha afya za wananchi kwa kuwakutanisha pia na madaktari bingwa wakimo kutoka hospitali ya Aghakhan.

“Wananchi wa Shinyanga jitokezeni kwa wingi kwenye kampeni hii kupima afya zenu pamoja na kupata matibabu bure,”amesema Macha.
Aidha,amempongeza pia Rais Samia kwa kuboresha huduma za afya hapa nchini na Mkoa wa Shinyanga ambapo kwa kipindi chake hadi sasa ametoa kiasi cha Sh.bilioni 30 na zimejengwa hospitali mpya zahanati na vituo vya afya lengo ni kuimarisha afya za wananchi.

Amewata pia wananchi wa Shinyanga kukata kadi za bima za afya ambazo zitawasaidia pia kupata matibabu kwa urahisi pamoja na kujitoa kuchangia damu.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile, amesema kampeni hiyo ya afya code clinic zinatolewa pia elimu za afya pamoja na uchunguzi wa magonjwa mbalimbali na hivyo kuwasisitiza wananchi wachangamkie fursa hiyo.

Naye Meneja Mkuu wa Jambo Media Nickson Geogre, amesema walizalisha wazo hilo kupitia vipindi vyao vya kijamii katika eneo la afya,ili jamii ipate kunufaika kwa kupata matibabu bure na wasikilizaji wao wawe na afya njema.
Nao baadhi ya wananchi ambao wamejitokeza kupata matibabu bure, wameishukuru kampuni ya jambo pamoja na Serikali, kuwapatia huduma hiyo na kuokoa afya zao.

Kampeni hiyo ya matibabu bure afya code clinic imeanza jana julai 24 na itahitimishwa julai 27 mwaka huu ambayo ni siku ya jumamosi

TAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye uzinduzi wa kampeni ya afya code clinic.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk.Yudas Ndungile akizungumza kwenye kampeni ya afya code clinic.
Meneja Mkuu wa Jambo Media Nickson Geogre akizungumza wazo la kuanzisha kampeni hiyo ya afya code clinic kutoka kampuni ya Jambo Group.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akipima afya kwenye kampeni hiyo ya afya code clinic.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungukia Mabanda mbalimbali ambayo yanatoa huduma za afya kwenye kampeni hiyo ya afya code clinic.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiendelea kuzungukia Mabanda mbalimbali ambayo yanatoa huduma za afya kwenye kampeni hiyo ya afya code clinic.

Huduma za kiafya zikiendelea kutolewa.
Huduma za kiafya zikiendelea kutolewa.
Huduma za kiafya zikiendelea kutolewa.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akiwasili kuzindua kampeni ya afya code clinic.
Wananchi wakiendelea kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni ya afya code clinic kwa ajili ya kupima afya zao na kupata huduma ya matibabu.

Post a Comment

0 Comments