DC MTATIRO ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI MWAMALILI
MKUU wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro,amefanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi Wamalili Manispaa ya Shinyanga na kuzitafutia ufumbuzi.
Mkutano huo umefanyika leo Julai 8,2024 kijijini humo na kuhudhuriwa na Watalaamu mbalimbali wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na Taasisi za Serikali, ili kutoa majibu ya kero ambazo zitawasilishwa na wananchi kwenye mkutano huo.
Mtatiro akizungumza na wananchi hao,amesema ameletwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, kuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ili kumsaidia kazi ya kusimamia miradi ya maendeleo pamoja na kutatua kero za wananchi.
“Nimeletwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan hapa Shinyanga, kuja kurekebisha mambo sehemu ambazo zimepinda pinda na kulegea legea ili kupanyoosha, sasa hapa Mwamalili kuna baadhi ya Sekta mambo hayaende vizuri ndiyo maana nimekuja kusikiliza kero zenu ili nizitatue,”amesema Mtatiro.
“Na hapa nilikuja pia kwa mambo mawili tu umeme na maji, lakini mmeibua na vitu vingine ambavyo naahidi kuvifanyia kazi, na huduma ya maji na umeme mtapata hivi karibuni tunakwenda kulifanyia kazi,”ameongeza Mtatiro.
Naye Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Said Kitinga akizungumza na wananchi kwenye Mkutano huo wakati akimkaribisha Mkuu wa wilaya kuzungumza na wananchi, ametoa wito kwa wananchi kwamba wajitume kufanya kazi ili wapate maendeleo kama alivyoelekeza Rais Samia, pamoja na kusomamesha watoto.
Diwani wa Mwamalili James Matinde,amesema kwenye Kata hiyo Rais Samia ametoa fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na changamoto zilizopo zipo kwenye mchakato wa kutatuliwa likiwamo suala la ukosefu wa maji hasa katika kijiji cha Bushora.
Nao wananchi wakiwasilisha kero kwa Mkuu wa wilaya, wametaja baadhi ya changamoto ambazo zinawakabili ikiwamo ya ukosefu wa huduma ya umeme,maji,upungufu wa Walimu, Wahudumu wa afya, kutolipwa fidia kwenye mradi wa SGR, ukosefu wa Josho la kuogeshea mifugo, na ubovu wa miundombinu ya barabara.
Afisa Tarafa ya Oldshinyanga Neema Mkangara akizungumza kwenye Mkutano huo.
TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julius Mtatiro akisikiliza na kuandika kero za wananchi wa Mwamalili kwenye mkutano wa kusikiliza kero zao na kuzitatua.