Header Ads Widget

RC MACHA:BIASHARA LAZIMA IWE MUHIMILI WA SERIKALI NA KULIPA MAPATO

RC MACHA:BIASHARA LAZIMA IWE MUHIMILI WA SERIKALI NA KULIPA MAPATO

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha,akizungumza kwenye kikao cha baraza la biashara la Mkoa huo,masema kwamba biashara lazima iwe muhimili wa Serikali pamoja na wafanyabiashara kulipa mapato.

Amebainisha hayo leo Julai 17,2024 wakati akifungua kikao cha baraza la biashara la Mkoa wa Shinyanga.
Amesema huwezi kuzungumzia maendeleo bila ya kutaja tozo, na hivyo kuwataka wafanyabiashara wa Mkoa huo kwamba wafanye biashara zao,lakini wazingatie taratibu za nchi ikiwamo kulipa mapato ya Serikali.

“huwezi kuzungumzia suala la maendeleo bila tozo, nawasihi wafanyabiashara waendelee kulipa mapato ya serikali,na tunampongeza Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameendelea kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara ikiwamo kuondoa tozo ambazo ni kikwazo,”amesema Macha.
“Na sisi katika Mkoa wa Shinyanga tutaendelea kujadili na kutatua changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili wafanyabiashara,pamoja na kuhakikisha wanaendelea kulipa tozo,lakini tozo ziwe rafiki ili kulinda biashara zao na wapate faida,”ameongeza Macha.

Aidha,amelitaka baraza la biashara la mkoa huo kuunda Kamati ambayo pia itakuwa ikijadili fursa za kuimarisha ustawi wa biashara,pamoja na biashara hizo zikidhi mahitaji ya wananchi.
Pia,amekemea tabia ya wafanyabiashara kuwaibia wananchi hasa katika suala la uchakachuaji wa kilo pamoja na kuuza bidhaa bei juu,tofauti na waliponunua wao kwenye masoko ya jumla na kuja kumfanyia wizi mlaji wa mwisho hasa kwenye sukari na mafuta ya kupikia.

katika hatua nyingine ameagiza kuimarishwa kwa masuala ya kilimo biashara pamoja na ufugaji,kwa wakulima kupewa elimu sahihi namna ya kufanya kilimo biashara na kuinuka kiuchumi likiwamo zao la Pamba.
Naye Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka Kanda ya Ziwa Andrew Kimbelwa,akiwasilisha mada kwenye kikao hicho,amesema wamekuwa wakisaidia wakulima kupata mikopo kupitia benki za biashara kutokana na dhamana zao hazitoshelezi.

Amebainisha kwamba wameshatoa Sh.bilioni 200 kwa taasisi za kifedha 16 ili kuwakopesha wakulima,na kwamba katika Mkoa wa Shinyanga wameshatoa fedha za mkopo zaidi ya bilioni 73.5 ikiwamo kujenga viwanda,kutoa pembe jeo,ufufuaji viwanda,kutoa fedha za mitaji, na wakulima zaidi ya 50 wameshanufaika na mikopo hiyo pamoja na kutoa ajira.
Kwa upande wake Meneja Wakala wa usalama na afya Mahali pa kazi (OSHA)kutoka Kanda ya Ziwa Mhandisi Lodgard Bishanga, akichangia mada kwenye kikao hicho,amesema Serikali ya Rais Samia inawathamini wafanyabiashara na kwamba imeshafuta tozo 11 ambazo zilikuwa kikwazo zenye thamani ya Sh.bilioni 35 kwa mwaka.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anamringi Macha akizungumza kwenye kikao hicho.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof Siza Tumbo akizungumza kwenye kikao hicho.
Meneja mradi kutoka Shirika la Solidaridad Winfrida Kanwa akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka Kanda ya Ziwa Andrew Kibembelwa akiwasilisha mada kwenye kikao hicho.
Kikao cha Baraza la Biashara cha Mkoa wa Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Biashara cha Mkoa wa Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha Baraza la Biashara Mkoa wa Shinyanga kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments