CRDB BENKI KUFANIKISHA MALENGO YA WAFANYABIASHARA -SHINYANGA.
Na Shaban Alley.
Benki ya CRDB kuendelea
kuimarisha mahusiano na wateja wake wa muda mrefu mkoani wa Shinyanga ili
kuwapa fursa mbalimbali za benki katika kufanikisha malengo ya wafanyabiashara
hao.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa benki ya CRDB, Bw. Abdulmajid Nsekela wakati akiwa katika ziara ya
kutembelea wateja wa benki hiyo mkoani Shinyanga ndani ya wiki hii.NSekela
amewahakishia wateja hao kuwa benki itaendelea kuimarisha huduma na bidhaa za benki ili wafanikisha
malengo ya wafanyabiashara.
Nsekela amekutana na wafanyabiashara
makundi mbalimbali ndani ya mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya mazungumzo ya kibiashara.
Miongoni mwa wateja waliotembelewa na benki ya CRDB ni Bw, Jackton Koyi mmiliki
wa shule za KOM mkoani shinyanga.
“KOM –class ni moja ya wateja wetu wa muda mrefu ambaye kampuni yake
inajishughulisha na uuzaji, utengenezaji, usambazaji vifaa vyote vinavyohusiana
na kompyuta huku pia wamiliki kituo cha mafunzo ya kompyuta mjini shinyanga
“anasema Nsekela
“Niendele kukaribisha wafanyabiashara
wakubwa kwa wadogo kufika katika matawi yetu kwani tuna bidhaa na huduma
zinazolenga mahitaji ya makundi mbalimbali ya Wafanyabiashara. Anasema Nsekela.
CRDB benki imekuwa katika wakati mzuri wa kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa mkoa wa Shinyanga ili kuwajengea mazingira salama ya kibiashara kwa kuendelea kutumia bidhaa na huduma za benki hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa KOM –Class Limited,Bw.Jackton
Koyi ambaye anamiliki shule ya msingi na
sekondari ya KOM, ameeleza kuwa benki hiyo ilikuwa ni msaada kwake katika
uwekezaji alioanza toka mwaka 2006 kwa
mradi wa shule ya sekondari na kufanikisha wahitimu elfu ishirini na moja(21,000)