Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Dr Samia Katambi Cup imeanzisha mashindano ya kipekee ya kuibua vipaji vilivyojificha ambayo yatafanyika katika jimbo la Shinyanga mjini Mkoani hapa ambayo yatafadhiliwa na mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Patrobas Katambi.
Akizungumza leo na viongozi mbalimbali wa kata, wilaya, kamati ya michezo na wachezaji wa michezo mbalimbali katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini, Katambi amesema mashindano hayo yatasaidia kuibua vipaji mbalimbali kuanzia kwa vijana hadi wazee katika manispaa ya Shinyanga.
"Tumefanya na tumeamua kwa pamoja kuanzisha michezo hii kuanzia uongozi wa serikali ngazi ya wilaya hadi kata, hivyo tunashirikisha watu wengi kwani wananchi wa Shinyanga mjini walitamani sana kuona tunakuwa na mashindano ambayo yataamsha vipaji vyetu"amesema Katambi.
"Na tunafanya hivi ili tujumuishe watu wengi zaidi wanawake kwa wanaume, wazee na vijana na kuhakikisha kuwa na washiriki waliobora, washindi bora ambao watatujengea katika ukanda wetu wa kanda ya ziwa, kwani yataamsha ari, kufahamiana na kutambuana,"ameongeza Katambi.
Aidha amesema timu nyingi katika maeneo mbalimbali zinakuwa hazina wazawa, kwa sababu ya kutoibua vipaji kuanzia chini, hivyo kuanzishwa kwa mashindano haya kutasaidia kupata vijana mbalimbali wenye vipaji vya aina tofauti.
"Shinyanga inawasanii wakubwa akiwemo Johari na marehemu kanumba na wengine wengi, ambapo tunatarajia kumwalika Johari katika siku ya uzinduzi wa mashindano haya, kwani sisi kazi yetu kwa sasa ni kuibua vipaji na kuvichokoza kwenye kila maeneo
hata kama ni rede audrafiti tutatoa ushirikiano ili waweze kufika mbali hata marekani inapobidi,"anesema Katambi.
"Tumeanzisha mashindano haya baada ya kufanya maendeleo kwa asilimia 99.5, katika manispaa ya Shinyanga hivyo kwa sasa tuko sawa kuanzisha mashindano kutokana na miradi mingi kutekelezeka, kutokana na Rais Samia kutuletea fedha nyingi za maendeleo na kuzisimamia ipasavyo,ameongeza Katambi
Kwa upande wake mwenyekiti wa mashindano hayo Yusuph Mbundi amesema mpaka sasa wana timu 32 za michezo na tayari wamekagua viwanja vyote vya mpira wa miguu na viwanja vya ngoma
Mratibu wa mashindano hayo Samwel Jackson amesema katika michezo hiyo wanataka watu wa kuanza nao na kumaliza nao hawataki watu wa kuvuruga, na michezo hiyo ni kwa ajili ya wananchi wa manispaa ya Shinyanga tu wanawake wazee na vijana, na kila kata itacheza, hivyo amewaomba wawe wakweli wasifanye udanganyifu kama kuna mchezaji amesajiliwa sehemu furani asijisajili sehemu nyingine
Baadhi ya wananchi wa Shinyanga akiwemo Ditrick Richard wamesema wanamshukuru mbunge kwa kuwa na maono makubwa ya kuanzisha mashindano hayo kwani itasaidia vijana wengi kuibua vipaji vyao pia itasaidia kujenga afya kwa wazee na vijana, kwani michezo ni afya.
Mashindano hayo yanatarajiwa kuanza Jumapili Julai 14/2024 katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Shinyanga mjini, ambapo michezo hiyo itashiriki katika kata zote za manispaa hiyo mpaka Julai 22 na Julai 23/2024 itakuwa ni mapumziko
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na viongozi na wanamichezo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na viongozi na wanamichezo
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na viongozi na wanamichezo
Viongozi wa mashindano ya Dr Samia Katambi wakimsikiliza mbunge Katambi akizungumzia mashindano hayo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464