KATAMBI, TUMETEKELEZA KWA ASILIMIA 99.9 SHINYANGA MJINI


Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,


Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi leo amezungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo, ambapo pia amewataka waendelee kuyasemea maendeleo makubwa yaliyofanyika katika awamu ya sita, ambayo yametekelezwa kwa asilimia 99.9

Hayo ameyasema leo Julai 12, 2024 wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata katika kata ya Ndala manispaa ya Shinyanga, ambapo amewataka viongozi wote waendelee kuzisemea kazi za maendeleo zlizofanywa na zinazoendelea kufanyika katika wilaya ya Shinyanga mjini.

Katambi amesema katika awamu ya sita wametekeleza miradi mingi ya kijamii kwa asilimia 99.9 katika manispaa ya Shinyanga, ambapo wamefanikiwa kujenga zahanati 6 vifaa tiba miundombinu ya barabara, madarasa na miradi mbalimbali ya kijamii, ambapo wananchi sasa hawana changamoto kubwa nyingi zimetatuliwa na zilizopo zinaendelea kutatuliwa.

"Leo nipo hapa kwa ajili ya kuweka utaratibu wa kueleza utekelezaji wa maendeleo yetu ya wilaya, tuliyoyafanya katika awamu ya sita niseme tena tumetekeleza kwa asilimia 99.9,"amesema Katambi.

Akisoma taarifa za miradi ya maendeleo diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole amesema kwa kushirikiana na Mbunge Katambi wametekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo zikiwemo Zahanati, madarasa, Hospitali, miundombinu ya barabara, umeme na miradi mbalimbali ya kijamii

Diwani wa kata ya Mwawaza Juma Nkwabi amesema tumefanya mambo mengi mbalimbali ikiwemo barabara ya kutokea Chibe na kutokea Old Shinyanga, kabla ya hapo watu walikuwa wakipata shida ya kuzunguka lakini kwa sasa wamerahisishwa hivyo wanamshukuru sana Rais kwa kuendelea kuwapambania wananchi.

"Na sasa kata ya Mwawaza inautajili wa Hospitali ya rufaa ambayo imeleta manufaa makubwa sana kwa wananchi, kuna biashara mbalimbali zinaendelea kufanyika,hivyo kwa sasa tunaomba tujengewe jengo la Mochwari kwani
wananchi wanapata gharama mara mbili, hivyo tunakuomba mbunge wetu utusaidie ili tuweze kupata Mochwari, katika hospitali yetu,"amesena Juma

Naye diwani wa kata ya Masekelo Peter Koliba amesema kwa ushirikiano mWamejenga madara , na matundu ya vyoo hivyo tupo vizuri tumekamilisha madarasa 20 na tumepata fedha zingine kwa ajili ya madarasa matatu, tumejenga kivuko watu wanapita bila shida, tumejenga Zahanati na watu wanaendelea kuhudumiwa ikiwa ni pamoja na miradi mingi mbalimbali ya kijamii tumefanikiwa

Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shabani amesema anamshukuru Rais Samia kwa kufanya mafanikio makubwa Zaidi ya milioni 200 zimetumika katika kata ya Ndala kwa ajili ya maendeleo Mbalimvali katika sekta za elimu,afya miundombinu ya barabara milioni 40 imetengwa kwa ajili ya kukamilisha Soko hilo amvalo limedumu kwa zaidi ya miaka 20 bila kufanyiwa ukarabati wowote

Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka amesema wanaomsema vibaya mbunge Katambi wanyamaze, maana mbunge anafanya mambo makubwa kwa kushirikiana na Rais Samia, lakini bado watu wanabeza, hivyo wananchi wote wanatakiwa kumpa mauwa yake mbunge Katambi na Rais Samia

"Tunakushukuru sana mbunge wetu kwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa ajili ya maendeleo makubwa yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika,tunamshukuru sana Rais wetu Samia Suluhu kwa kutupatia fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo Kwani kila kata imefikiwa, tunamshukuru diwani kwa kuendelea kutupigani, tunamkubali ni jembe lenye makali

Diwani wa kata ya Ndembezi Victor amesema kwenye kata ya Ndembezi tumefanya mambo makubwa sana ambayo yalikuwa hayapo lakini kwa sasa yapo , barabara zilikuwa hazipitiki lakini kwa sasa zinapitika, hivyo aliwaomba wananchi wamuombee mbunge na Rais ili waendelee kuwa na afya njema waendelee kwatumikia wananchi.

"Tunaomba utufikishie ujumbe kwa mama Samia kwamba wanawake wa Shinyanga wamefunga vibwebwe wapo bega kwa bega na Rais Samia,kwa sababu wameziona kazi zake, amesema Sheila Mshandete.


Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,
Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza katika kata ya Ndala
Wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ndala Joel Kaholwe akizungumza
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Hamisa Chaha akizungumza kwenye kikao cha wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,

Katibu Muenezi wa Wilaya Said Bwanga akizungumza
Wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo,
Mbunge viti maalum Pascazia Seni akizungumza
Diwani viti maalum manispaa ya Shinyanga Sheila Mshandete akizungumzia maendeleo yaliyofanyika
Diwani viti maalum manispaa ya Shinyanga Ester Makune akizungumza
Diwani wa kata ya Kizumbi Reuben Kitinya akizungumza kwenye halmashauru kuu za kata
Diwani wa kata ya Ndembezi  Viktor Thobias Mmanywa akizungumza 
Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza na kuwaombea msamaha wale wote wanaobeza kazi zilizofanywa na Rais kwa kushirikiana na mbunge
Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumzia miradi ya maendeleo iliyofanyika
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Ndala, Kambarage, Mwawaza na Masekelo
Madiwani wakitoa taarifa ya maendeleo





Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464