Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza na halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga
Suzy Butondo, Shinyangapress blog
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi amehitimisha ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na halmashauri kuu za kata 17 katika wilaya ya Shinyanga mjini,ambapo amewataka viongozi wote kuhamasisha watu wakajiandikishe kwenye daftari la kudumu ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Akizungumza na halmashauri kuu za kata za Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga amesema lengo lake ni kukutana na halmashauri kuu za kata katika wilaya ya Shinyanga mjini ili kueleza kazi zilizofanywa na Rais Samis Suluhu Hassan katika awamu ya sita.
Amesema toka aingie madarakani Rais Samia amefanya kazi kubwa ametoa fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo kulikuwa na changamoto za barabara, maji, zahanati lakini changamoto hizo zimetatuliwa wananchi wanapata huduma kwa karibu na sasa kuna fedha za kuchimba visima saba vya maji ambavyo vitachimbwa kwenye maeneo ambayo hayajafikiwa na maji ya ziwa victoria.
"Kwa kweli hatuna budi kumuunga mkono na kumshukuru mama yetu mama Samia Suluhu kwa kazi kubwa anazozifanya, na sasa nimepata visima saba vya kuchimba kwenye maeneo ya kata ambazo zinapata shida na nitaangalia maeneo na taasisi ambazo hazijafikiwa na maji, tukijumlisha na vilivyopo vitakuwa saba"amesema Katambi
Aidha diwani wa kata ya Mwamalili James Matinde alielezea miradi mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika kata yake, ambapo pia amemshukuru Rais Samia Suluhu kwa kushirikiana na mbunge katambi katika kufanya mabadiliko makubwa katika kata na Taifa kwa ujumla.
"Kwa kweli Mungu ambariki Katambi kwa juhudi kubwa anazozifanya katika jimbo letu, kwani sio mtu wa kukaa wala kulala anatambua kuwa ni mwakilishi wa wananchi ndiyo maana tunayaona haya mabadiliko makubwa katika kata, wilaya na Taifa, hivyo tuwaunge mkono viongozi wetu, ikiwa ni pamoja na mama mchapakazi mama Samia Suluhu Hassan,"amesema Matinde.
Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Shinyanga Joseph Hundaha na Herena Ngeleja wamesema wanampongeza mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi kwa kuleta maendeleo makubwa katika jimbo la Shinyanga mjini hivyo wameahidi kumuombea ili aweze kuleta maendeleo makubwa katika jimbo lake
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza na halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza na halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga
Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na wenye ulemavu, Patrobas Katambi akizungumza na halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha akizungumza na halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga
Diwani wa kata ya Mwamalili James Matinde akielezea miradi ya mbalimbali ya maendeleo iliyofanyika katika kata yake
Wajumbe wa halmashauri kuu za kata ya Lubaga, Mwamalili, Chibe na Oldshinyanga wakimsikiliza mbunge wa jimbo hilo Patrobas Katambi

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga wakiwa kwenye kikao
Diwani viti maalum Picca Chogelo akizungumza kwenye kikao hicho
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464