Watalaamu kutoka vitendo tofauti sekta ya Afya wakiwa katika mdahalo wakielezea namna walivyopunguza vifo vya watoto wachanga mkoani Shinyanga.
Na Kareny Masasy,
SABABU ya vifo kupungua Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga nikutokana na serikali kuwa na mipango madhubuti pamoja na kuungana na wadau mbalimbali wanaotekeleza kupunguza vifo vya watoto wachanga na wajawazito.
Sera ya afya ya mwaka 2007 imewekeza katika kuboresha uhai wa mtoto kupitia utoaji wa huduma za afya bure kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Uwekezaji wa serikali katika uhai wa mtoto unaonekana dhahiri kwenye kupungua kwa vifo vya watoto kati ya mwaka 2010 hadi 2015 ambapo kiwango cha vifo vya watoto wachanga kuanzia siku 0 hadi 28 vimepungua kutoka vifo 40 hadi vifo 25 kwa kila kizazi hai 1000.
Mratibu wa afya ya Mama na Mtoto mkoani Shinyanga Halima Hamis anasema kumekuwepo na vituo vya kutolea huduma ukijumlisha na hospitali za Halmashauri na Rufaa 243 na vyote vinahuduma ya mama na mtoto bure.
Pia mkoa huu kuna vituo 35 vya kutolea huduma ambapo vituo vya afya pekee viko 25 na Hospitali ni 10 ambapo mahudhurio ya kliniki kwa mjamzito wiki ya 12 za mwanzo yamefikia asilimia 34 ukilinganisha na kitaifa asilimia 60 yapo mafanikio.
Hamis anasema kuongezeka kwa vituo vinavyotoa huduma ya dharura ya upasuaji kwa wajawazito katika kila kata kwa mujibu wa sera ya afya ya mwaka 2007 inavyoeleza.
“Ipo huduma ya M-Mama ambayo ilikuwa ikifadhiliwa na Mdau na sasa Halmashauri ndizo zimechukua jukumu hilo baada ya Mdau kuisha mkataba wake”anasema Hamis.
“Halmashauri hizo zimekuwa zikitenga fedha kwaajili ya kusafirisha wajawazito na watoto wenye changamoto kwa utaratibu wa kushirikiana na viongozi wa mtaa,vitongoji,vijiji ambapo wao ndiyo wanatafuta gari na dereva wanao waamini na malipo yanalipwa kutoka Halmashauri”anasema Hamis .
Halima anasema mpango wa M-Mama ulianza katika halmashauri wilaya ya Shinyanga kama majaribio kwa mwaka mmoja ikaonekana kufanya vizuri na sasa mpango huo upo kwenye halmashauri zote sita za mkoa.
Halima anasema njia ya uzazi wa mpango inazuia vifo kwa asilimia 40 ambapo kila Zahanati au kituo cha afya kuna huduma hiyo wanapokwenda kliniki wanapewa elimu.
Wadau wanaotekeleza uzazi wa mpango kwa mkoa wa Shinyanga ni Mariestopes na Pathifinder wamekuwa wakishirikisha baba na mama katika utoaji elimu
Pia kuna Mradi wa kitita salama una mdau wake na Thamini uzazi Salama nao mdau wake wenye malengo ya kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto kutoka hospitali ya Rufaa ya Mkoa Justina Tizeba anasema asilimia 10 ya watoto wanaozaliwa wanahitaji kusaidiwa zaidi wengine wanazaliwa njiti.
Dk Tizeba anasema sababu ya vifo vya watoto wachanga vinazuilika kina baba nao washirikiane na mama katika huduma ya mtoto pindi bado mchanga.
Daktari bingwa wa Magonjwa ya wanawake kutoka hospitali ya rufaa ya Mkoa Dk Agustino Maufi anasema asilimia 57 ya wanawake wanaobeba mimba wanakuwa na viashiria vya upungufu wa damu.
Dk Maufi anasema mpango uliokuja umeongeza mahudhurio ya kliniki kwa wajawazito badala ya mahudhurio manne yamekuwa nane nakuhakikisha kila hudhurio anapimwa wingi wa damu.
“Mjamzito huyo ataweka mahusiano mazuri na watoa huduma na atakapo hudhuria kliniki mara zote hawatapata changamoto nakuendelea kuokoa vifo vya watoto wachanga”anasema Dk Maufi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Annamringi Macha anasema kwa kipindi cha miaka mitatu serikali imeleta zaidi ya Shilingi Bilioni 30 kwenye sekta ya afya na kumekuwepo ongezeko la vituo vya afya 37 Zahanati 50 nakufikia vituo vya kutoa huduma ndani ya mkoa 270.
Waziri Afya Ummy Mwalimu anaeleza kuwa ongezeko hilo la matumizi ya huduma za kliniki wakati wa ujauzito limetokana na kubadilika kwa mwongozo wa huduma muhimu wakati wa ujauzito kutoka mahudhurio ya kila baada ya miezi mitatu na kuwa mahudhurio ya kila mwezi.
Pia kuna Kuongezeka la wahamasishaji ambao ni wahudumu ngazi ya jamii kuanzia ngazi za vitongoji juu ya uhumimu wa wajawazito kuhudhuria kliniki .
“Takwimu zinaonesha kuwa kati ya wajawazito 1,784,809 ni wajawazito 656,040 sawa na asilimia 37.6 walianza kupata huduma za wajawazito chini ya wiki 12 za mwanzo wa ujauzito ikilinganishwa na asilimia 36 ya kipindi kama hiki mwaka 2020,” ameongeza.
Malesela anasema Manispaa ya Kahama Vituo sita vimepata wahudumu waliopitia mafunzo na kupitia mradi wa Kitita cha Uzazi Salama (SBBC) wadau hao wameajiri watu wanaofuatilia takwimu za mama wanaojifungua salama pamoja na watoto na waliopoteza maisha pia .
“Takribani kwa siku watoto wanazaliwa kwa hospitali ya manispaa ya Kahama ni 35 hadi 40 na kwa mwezi watoto zaidi ya 1000 na kila mtoto anaweza kuzaliwa na changamoto zake”anasema Malesela.
Watoto wengi wametambulika na kupona ndiyo maana tulikuwa tunaendelea kuona vifo vya watoto wachanga vinazidi ikiwa mwaka 2020 kulikuwa na vifo 382 vya watoto wachanga.
Zubeda Galula mkazi wa Manispaa ya Kahama Kata ya Majengo anasema alipata changamoto ya uzazi wakati anajifungua akapata rufaa ya kusafirishwa kuletwa Shinyanga mjini amefurahi kuokolewa yeye na mtoto wake.
Mariamu Joshua ambaye ni wifi yake Zubeda anasema alielezwa awali kabla ya kujifungua njia haifunguki lakini waliona wauguzi hali inazidi kuwa mbaya walimsafirisha na sasa anaendelea vizuri na mtoto.