MWENYEKITI UVCCM MKOA WA SHINYANGA, "SITAKUBALI KUONA KIJANA ANAMSEMA VIBAYA KIONGOZI ALIYEKO MADARAKANI"


Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Benard Werema akiwa na viongozi baada ya kupokelewa na UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini akiwasili katika ofisi za CCM wilaya hiyo

Suzy Butondo, Shinyanga, shinyangapress blog

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana UVCCM mkoa wa Shinyanga Benard Benson Werema amewataka vijana kuacha kuwasema vibaya viongozi waliopo madarakani badala yake washirikiane na wawaunge mkono kwa kazi kubwa wanazozifanya za kuleta maendeleo.

Hayo ameyasema leo 30,2024 wakati akizungumza na wajumbe wa baraza la umoja wa vijana Shinyanga mjini, ambapo amewataka vijana kuacha kuwasema vibaya viongozi walioko madarakani, washirikiane nao ili waweze kutimiza malengo yao waliojiwekea ya kuleta maendeleo.

"Sitakubali kuona kijana anamsema vibaya kiongozi wake aliyeko madarakani, tuwaache viongozi wetu watimize wajibu wao, tuachane na mihemko ya kubebelea wagombea tuwaache viongozi wetu watekeleze yale waliyoahidi, tusubiri wakati ukifika kila mmoja atapambana,"amesema Werema.

"Niwaombe tuwe wazalendo kama viongozi waliopo madarakani wanafanya vizuri wachaguliwe tena ukifika wakati wa uchaguzi, lakini kwa sasa mnatakiwa kushirikiana nao, ole wako upokee kimemo kuja kumchagua mtu ambaye usiyemjua waacheni watu wakamchague mtu wanae mtaka wao wenyewe, usikubali kupokea memo yoyote ukawaacha viongozi wanaotakiwa"ameongeza.

Amesema serikali kwa kushirikiana na viongozi inapambana kuhakikisha inatekeleza miradi mbalimbali katika nchi, hivyo kazi ya vijana ni kuyasema yale maendeleo yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika ili kuipunguzia kazi serikali, na kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.

"Rais wetu Samia Suluhu ametoa fedha nyingi kwa ajili yakutekeleza miradi mbalimbalo,hivyo niwaombe miradi hiyo tuitunze asitokee mtu wa kuihujumu miu dombinu mbalimbali iliyotengenezwa, atakayetokea mtu wa kuhujumu atachukuliwa hatua kali za kisheria,"amesema Werema.

Pia amemuagiza katibu wa UVCCM mkoa wa Shinyanga kuhakikisha anaandaa kikao cha uchaguzi ili aweze kuchaguliwa mwenyekiti wa UVCCM wilaya kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha amewataka vijana wakae vizuri na waweze kuwa waadilifu na wasimame imara wasiteteleke, wajitoe wahakikishe wanatekeleza wajibu na wakaimarishe kamati zao zote na kutekeleza yale waliyoelekezwa.

"Niwaombe vijana sisi tuliojitoa tuhakikishe tunatekeleza wajibu wetu kupitia kikao hiki twendeni tukaimarishe jumuiya yetu, na tutengeneze utaratibu wa kuchaguana si kupangana tu na niwaase kwamba unapokuwa kiongozi lazima ubadilike na kuna mambo lazima uyaache kuwa mnyenyekevu, nidhamu na muadilifu usiwe na mhemuko wa kufanya jambo,"amesema Chacha

Amesema tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani kuna mambo mengi ya kisekta ambayo ameyafanya hivyo wakayasemee vizuri, kuwaomba wakajitokeze kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mjumbe wa baraza Taifa Monalisa Daniel amesema vijana wanatakiwa kuwa wabunifu wajiendeleze kielimu na wapende kujisomea misingi mbalimbali, ili hata wamapokutana na maswali waweze kuyajibu kwa usahihi.

"Niwaombe vijana wenzangu tuepuke kujiingiza kwenye makundi yasiyofaa safari ya maisha yako ni wewe mwenyewe vikemee vitu vinavyokufanya ujiingize kwenye vikundi hivyo, tuendelee kukisema chama pale tunapokoseana tusameheane, tutambue wajibu wetu,tukailinde amani na tukawe askari wazuri kwwni kuna watu wsnarawitiwa wanabakwa na watoto kibiwa, tutoe taarifa tunapoona matukio ya namna hiyo"amesema.

Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga akizungumza na vijana wa Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga akizungumza na vijana wa Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga akizungumza na vijana wa Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga akisalimiana na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha
Mwenyekiti wa umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga akikabidhiwa zawadi ambàyo ni picha yake  na katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha
Severine Luhende ambaye ni hamasa wa Mkoa wa Shinyanga kaizungumza
Monalisa Daniel mjumbe wa baraza Taifa akizungumza
Katibu wa Umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga 
Katibu wa Umoja wa UVCCM mkoa wa Shinyanga 
Katibu wa Umoja wa UVCCM wilaya ya Shinyanga mjini Naibu Katalambula akizungumza




Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha akizungumza
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Hamisa Chacha akizungumza
Katibu wa Mbunge wa jimbo la Shinyanga Samueli Jackson akizungumza

Mwenyekiyekiti mstaafu wa UVCCM wilaya ya Shinyanga Dotto Joshua akizungumza
Wajumbe wa baraza wakimsikiliza mwenyekiti
Wajumbe wa baraza wakimsikiliza mwenyekiti
Wajumbe wa baraza wakimsikiliza mwenyekiti
Wajumbe wa baraza wakimsikiliza mwenyekiti









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464