Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT hiyo
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake UWT CCM wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo amewataka wajumbe wa baraza la UWT kuachana na makundi badala yake watumike kwenye nafasi zao walizochaguliwa kufanya, na kuwasemea viongozi waliopo madarakani kwa kazi walizozifanya katika awamu ya sita.
Hayo ameyasema jana kwenye kikao cha baraza la Umoja wa wanawake UWT wilaya ya Shinyanga, ambapo amewataka wajumbe wa baraza hilo waachane na makundi ambayo yanaweza kuleta mipasuko ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
"Niwaombe wanawake wenzangu tuachane na mambo ambayo hayatuhusu, tufanyeni kazi zetu kwa kushirikiana na madiwani, wabunge walioko madarakani,na tuwasemee kwa maendeleo makubwa waliyoyafanya kwa asilimia 99,amesema Nhamanilo.
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo amewataka viongozi wote waache kutembea na wagombea wao mifukoni kwa sababu madiwani wapo na wabunge wapo wawaache wafanye kazi zao wasiwadhoofishe.
"Tumeviweka vidiwani vibunge vidogo vidogo tunatembea navyo tuacheni, kuwakimbiza kimbiza madiwani wetu na wabunge jamani, kwanza sijaona mbunge ambaye hatoshi kwenye mkoa huu wote wana tosha, hivyo ni vizuri ukiwa na imani kwa kila mtu,Shinyanga tuna nidhamu tuendelee kuwa na nidhamu hiyo hiyo,"amesema Batimayo.
"Pia niwakumbushe wanawake msisahau majukumu yenu ya malezi, kuhudumia wenza wenu na muweze kutenga muda wa kuzungumza na watoto wenu katika kuwafundisha maadili mema.
"Muda wa kuandaa wabunge na madiwani tunaupata wapi, kinachotakiwa tupendane tushikamane tuheshimiane, na tusubiri muda ukifika tutafanya ya kwetu, lakini kwa wakati huu tulionao tuheshimu viongozi wetu walioko madarakani, tuko kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, twendeni tukahamasishe wananchi wote wajiandikishe ili waweze kupata haki ya kupiga kula, tusijisahau na kina mama nendeni mkawahamasishe wajitokeze kwa wingi kugombea"ameongeza.
Aidha mbunge wa jimbo la Shinyanga Patrobas Katambi ambaye pia ni
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu
amewataka wananchi waendelee kulinda amani wasiipoteze, ambayo ipo kwa sababu chama cha mapinduzi CCM kipo madarakani na kipo imara.
"Maendeleo yetu ni muhimu, kama kuna tofauti tuziweke kando tuendelee kuchapa kazi na niombe kikao hiki kikalete upendo,kikalete chachu ikiwa ni pamoja na kumpongeza mama yetu Rais Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo aliyofanya na anayoendelea kuyafanya, kikao hiki hakinihusu lakini nimepita tu kuwasalimia baada ya kusikia mnaendelea na kikao nawapenda, "amesema Katambi.
Naye mbunge viti maalum mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava amewaomba wanawake wapendane washirikiane kwa pamoja na wahakikishe wanahamasishana kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa.
"Tunapoelekea kwenye uchaguzi tuwahamasishe wanawake wenzetu wenye uwezo waweze kugombea nafasi mbalimbali za serikali za mitaa, na ukimuona mwanamke mwenzio anagombea umtie moyo, usimkatishe tamaa,pia tuendelee kuzisemea kazi zilizofanywa na Rais wetu Samia Suluhu bila kuwasahau wabunge wetu wa majimbo,"amesema Mnzava.
Hata hivyo wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga walionyesha upendo mkubwa kwa wabunge wao waliohudhulia kikao hicho kwa kuwabebba juu juu, kuonyesha ishara ya upendo ambao ni Patrobas Katambi na Christina Mnzava.
Baadhi ya wajumbe wa baraza hilo akiwemo Mariam Kajala amesema anawaomba wabunge hao waendelee na moyo huo, kwani wameonyesha upendo mkubwa kwa kuhudhulia baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini, na kuahidi kwamba maagizo yote yaliyotolewa katika kikao hicho watayatekeleza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,kazi,vijana,ajira na watu wenye ulemavu akizungumza
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza kwenye baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza kwenye baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akizungumza kwenye baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT hiyo
Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga mjini Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye kikao cha baraza la UWT hiyo
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga mjini Hamisa Chacha akizungumza
Wajumbe wa kamati ya utekelezaji wakiwa kwenye kikao hicho
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye baraza hilo
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye baraza hilo
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa kwenye baraza hilo wkiburudika pamoja na mbunge wa jimbo hilo patrobas Katambi
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akiburudika pamoja na wajumbe wa baraza Shinyanga mjini
Mbunge viti maalum Mkoa wa Shinyanga Christina Mnzava akiburudika pamoja na wajumbe wa baraza Shinyanga mjini
Wajumbe wa baraza la UWT wilaya ya Shinyanga mjini wakiwa wamembeba juu juu mbunge viti maslum Chritina Mnzava