TAKUKURU SHINYANGA KUTHIBITI VITENDO VYA RUSHWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, WABUNGE, MADIWANI NA MAWAKALA WABAINISHWA KATIKA RIPOTI.
Na mwandishi Wetu,
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa (Takukuru) mkoa wa Shinyanga imejipanga kuthibiti vitendo vya rushwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwaka huu (2024) kwa kutoa elimu kwa wadau juu ya madhara ya rushwa.
Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Shinyanga. BW. Damian Kessy ameeleza
hayo julai 31, 2024 katika mkutano wake na vyombo vya habari wakati akiwasilisha
taarifa yake kwa kipindi cha miezi mitatu yakuanzia April hadi Juni.
“Takukuru itatoa elimu
kwa wadau mbalimbali ikiwa ni wajumbe ambao ni wapiga kura, Wagombea,wasimamizi
wa uchaguzi, viongozi wa dini , waandishi wa habari na kutoa elimu kwa wananchi
wa kata zote 130 za mkoa wa shinyanga ili kuhakisha tunawajengea uelewa wa
kubaini vitendo vya rushwa kabla na wakati wa uchaguzi “anaeleza Kessy
Anaongeza pia “Takukuru
kuchukua hatua za kisheria pale itakapobainika Wagombea au wapambe wanajihusisha
na vitendo vya rushwa”
Hata hivyo Mwandishi wa Makala hii anaeleza uchaguzi wa
serikali za mitaa umekuwa na hali ya matukio ya mianya ya rushwa kwa kila nyakati
na hali inayofanya kudumaza kwa ukuaji wa demokrasia nchini na kutopatikana viongozi bora.
Mwandishi huyo anaeleza, Matokeo ya utafiti ya Takukuru juu
ya mianya ya rushwa katika uchaguzi wa mwaka 2014 yalibainisha viashiria vya
rushwa.
Kwa mujibu wa taarifa
ya mianya ya rushwa serikali za mitaa kupitia tovuti ya Takukuru inaonyesha kwa mwaka 2014, Wananchi walidai walishuhudia vitendo vya rushwa katika kampeni
za uchaguzi wa serikali za Mitaa 2014 ambapo, asilimia 54.2 walieleza kuwa
hakukuwa na vitendo vya rushwa na asilimia 42.9 walieleza kuwepo kwa vitendo
vya rushwa.
Tovuti hiyo ilionyesha
asilimia 32.9 ya wahojiwa walieleza kulikuwa na vitendo vya rushwa vilivyohusiana
na ugawaji wa fedha taslimu, asilimia 9.8 walieleza kuwepo kwa ugawaji wa kanga
na Tshirt na asilimia 26.8 walieleza kuwa wapiga kura walipewa vinywaji na
vyakula.
Kwa mujibu wa tovuti hiyo inaeleza utafiti wa mwaka 2014, ulibanisha
vitendo vya rushwa katika mchakato wa kampeni za serikali za mitaa na vitendo
hivyo vilivyohusisha ugawaji wa mifuko
ya saruji, ugawaji wa mipira ya miguu, harambee kanisani, kutoa pikipiki na
michango katika misiba.
Pia baadhi ya maeneo vitendo vya rushwa vilijidhihirisha kwa
ugawaji wa chumvi na vitu vingine vya thamani siku ya kupiga kura.
Pia ugawaji vitu vya rushwa kulifanyika kwa kupelekwa
majumbani kwa wapiga kura au wakati wapiga kura wanaelekea vituoni kupiga kura
na katika matukio hayo, utafiti ulibaini
shughuli hizo ziligharamiwa na baadhi ya
wagombea na katika baadhi ya maeneo, mawakala wa wagombea walitumika.
Mwaka huo wa uchaguzi ulionyesha baadhi ya maeneo madiwani na wabunge
walishirikiana na baadhi ya wagombea kuwahonga wapiga kura, Madiwani na
wabunge walishirikiana na wagombea kwa matarajio kuwa watakaposhinda
watawasaidia katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
MWISHO.