Header Ads Widget

TAKUKURU MKOA WA SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI VIONGOZI NANE AKIWEMO MENEJA WA KACU.



TAKUKURU MKOA WA SHINYANGA YAWAFIKISHA MAHAKAMANI VIONGOZI NANE AKIWEMO MENEJA WA KACU.

Na mwandishi wetu

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imewafikisha Mahakamani viongozi Nane wa vyama vya Msingi  AMCOS, akiwemo meneja wa Chama kikuu cha ushirika Kahama, (KACU) kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa vyombo vya habari leo Julai 31,2024 Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga Bwana Donasian Kessy amesema taasisi hiyo, imebaini kuwepo kwa vyama vya ushirika 13,vyenye madeni  yanayosababishwa na badhi ya viongozi kugushi nyaraka na wengine kutoa fedha kwenye akounti za Chama na kisha kuzigawana kupitia akounti  binafsi.

Amesema TAKUKURU imewabaini watuhumiwa hao kufuatia malalamiko ya wanachama wa chama cha Ushirika kahama Cooperative Union KACU,kukosa malipo baada ya kuuza mazao yao. 

Bwana Kessy amesema taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga imewafikisha mahakamani viongozi nane wa vyama vya Msingi vya Kangeme na Mshindi pamoja na Meneja wa KACU Abdul Ally kwa makosa hayo ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.

Ameeleza kuwa kesi nne zinaendelea mahakamani huku Jamhuri ikishinda katika shauri moja, ambapo watuhumiwa wameamriwa kulipa kiasi cha fedha shilingi Milioni 24, ambazo walizipata kwa njia ya rushwa na  kwamba tayari wamerejesha shilingi Milioni 12.

Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Shinyanga amesema taasisi hiyo inaendelea kushughulikia malalamiko katika vyama vingine 11,vya msingi AMCOS ili kuhakikisha hatua za kisheria  zinachukuliwa dhidi ya viongozi wote waliohusika
Taarifa hiyo ni ya utendaji kazi katika  robo ya Mwaka  iliyoanzia Mwezi April hadi June 2024.

Post a Comment

0 Comments