TAPO LA SHYEVAWC LIMEPITISHA MPANGO KAZI WA SHUGHULI ZA UTETEZI WA HAKI ZA WANAWAKE NA WATOTO KWA JULAI –DESEMBA 2024.
Na mwandishi wetu.
Kikundi cha asasi za kiraia mkoa wa Shinyanga kinachotambulika kwa jina la SHY EVAWC) kinachoshughulika na kutokomeza ukatili mkoa wa Shinyanga kimepitisha mpango kazi wake kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake kwa kipindi cha julai hadi desemba 2024. Kikundi hicho kinaundwa na asasi zipatazo 30 zinazotekeleza afua za MTAKUWWA kimekuwa ni msaada kwa jamii na serikali dhidi ya vitendo vya ukatili mkoa wa Shinyanga.
Mwenyekiti
wa TAPO la SHYEVAWC,Jonathan Kifunda
alisema ni wajibu kwa kila asasi
kuendelea na majukumu yake ya kutetea haki za wanawake na watoto kwa kuzingatia
Mpango kazi wa Taifa wa Kutomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na watoto(MTAKUWWA), Hayo yalibainishwa katika kikao cha robo mwaka cha kikundi kazi hicho
kilichiofanyika manispaa ya Shinyanga julai 2,2024.
“Mpango
kazi wa MTAKUWWA ni mpana sana na kila mwanachama analo jukumu la kuendelea
kutekeleza shughuli zake kwa kuchomoa kile anachoweza katika mpango huo wa
Taifa ili kusaidia serikali na jamii dhidi ya masuala ya ukatili kwa mkoa wetu”
TAPO
hilo limepitisha mpango kazi wake unajikita kutetea haki za wanawake na watoto
kupitia timu iliyogawanyika katika mihimili minne ikiwa ni uratibu(coordination),kuzuia(prevention), kutoa
huduma kwa wahanga(response) na mawasiliano kwa jamii(communications). Ambapo kila muhimili ulipata nafasi ya
kuwasilisha mpango kazi wake na kupatiwa baraka za wajumbe.
Wajumbe
wa TAPO hilo walionesha nia ya dhati ya kuwa na mikakati imara ya kuimarisha uendelevu
wa TAPO hili kwa kutoa maoni ili kufikia malengo waliyojipangia kwa ustawi wa maendeleo
ya utetezi wa haki za wanawake na
watoto.
Mjumbe
wa TAPO hili, John Shija alishauri chanzo za msingi wa kuwepo kikundi kazi
hicho ni kuendelea kutoa nafasi za watu walio na hiari zaidi na kujifunza zaidi
kwa wengine waliokwama ni vitu gani waliviweka na kuwafanya kukwama.
“Tulianza
kwa takafari kubwa juu ya TAPO hili kwa kutazama historia ya kufa kwa matapo
mengine na kuwa waangalifu katika kuepuka mambo yanayoweza kuwa ni kikwazo na
hadi leo tuko hapa,ni vema tukumbuke ile nia ya awali ili tuendele kuimarika “anasema
Shija.
Naye Catherine Kalinga kutoka kitengo cha utoaji
huduma kwa wahanga anashauri kuwepo na mfumo wa kidigitali wa ufatilia wa kesi
zote za ukatili kwa TAPO hili ili kuwa na kumbukumbu za matukio.
“Nishauri tuwe na mfumo rafiki wa pamoja utakaosaidia
kutambua mwanzo hadi mwisho wa kesi za ukatili ili tuwe na njia rahisi ya kufatilia”anasema
Kalinga
Kwa
upande wake Peter Amani kutoka Shirika la COED –Tanzania ameshauri ushirikiano
zaidi na vyombo vya habari baina ya kitengo cha mawasiliano na habari ili
kupaza sauti zaidi kwa utetezi wa haki za wanawake na watoto.
“Ni
vema tuendele kuimarisha mawasiliano kwa umma ili wajue shughuli zetu kwa upana
na tuwape mahitaji yao kwa wao kutambua akaunti zetu za mawasiliano za SHYEVAWC
na pia kuongeza wigo wa mashirikiano na vyombo
ya habari.
Pia
TAPO hilo liliweza kupokea wanachama wapya kwa ajili ya kujiunga kwa majukumu
ya utetezi wa haki za wanawake na watoto. Ambapo wanachama wapya Nacopha konga
manispaa ya Shinyanga, AGDC, na Lifeline walipokelewa.
Katibu wa NACOPHA KONGA,
Manispaa ya Shinyanga Edson Justine, Amesema ni muda muafaka wa kutokomeza
ukatili na unyanyasaji wa watu wanaishi na virusi vya ukimwi kwa kujiunga na
Tapo hilo.
Katibu wa NACOPHA KONGA, Manispaa ya Shinyanga Edson Justine,
Mkurugenzi wa shirika
la Life line,Dk. Kulwa Meshaki anasema,amekuwa na jitihada na kusumbua uongozi
ili ajiunge kwa kuona na kuridhika na makubwa yanayo fanya na kikundi kazi
hicho.
Mkurugenzi wa shirika la Life line,Dk. Kulwa Meshack akichangia mada
Mwamabadiliko kata ya pandagchiza, Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, Shadrack Ngome anasema yuko tayari kushirikia na SHYEVAWC ili kutoa elimu kwa jamii kupitia vikundi na mikutano ya hadhara.
Mwanamabdiliko ,Shadrack Ngome kutoka kata ya pandagchiza akijitambulisha kwa wajumbe.
MATUKIO KATIKA PICHA.
Katibu wa SHYEVAWC-Veronica Massawe akitoa maelekezo ya kikao cha robo mwaka cha SHYEVAWC
Vicent Laurent,Mwenyekiti wa uzuaji matukio ya ukatili akiwasilisha mpango kazi
Mwakilishi wa muhimili wa utoaji huduma (response) Catherine Kalinga, akiwasilisha mpango kaziMwakilishi wa timu ya uratibu,(coordination),Glory Mbia akiwasilisha mpango kazi.
Mwenyekiti wa muhimili wa mawasiliano na habari,(communications),Estomine Henry akiwasilisha mpango kaziTIMU ZA VIKUNDI-KUJADILI MPANGO KAZI-Muhimili wa uratibu (coordination) ukijadili mpango kazi.
muhimili ya kuzuia(prevention) ukijadili mpango kazi
Muhimili ya utoaji huduma (response)ukijadili mpango kazi.
WAJUMBE WAKICHANGIA MADA HAPA CHINI.
WAJUMBE WAKIFATILIA KIKAO-SHYEVAWC
WANAMBADILIKO KUTOKA NGAZI YA JAMII WAKITOA SALAM ZAO