WAKAZI ZAIDI YA MILIONI 1.9 KATIKA MIKOA SITA WANANUFAIKA NA MAJI YA ZIWA VICTORY- NAIBU WAZIRI WA MAJI.

 

WAKAZI ZAIDI YA MILIONI 1.9 KATIKA MIKOA SITA WANANUFAIKA NA MAJI YA ZIWA VICTORY- NAIBU WAZIRI WA MAJI.



Ofisi ya RUWASA  mkoa wa Shinyanga na ofisi ya Mbunge kishapu wakiwa katika tukio la kukagua huduma ya maji kwa wnanchi wa kishapu.



Na shaban Alley-
N
aibu waziri wa maji mhandisi Methew Kundo amesema hayo wakati alipotembelea chanzo cha maji cha mradi huo cha Ihelele kilichopo wilaya ya Misingwi mkoani Mwanza.

Naibu waziri amesema mradi huo mkubwa wa maji unanufaisha mikoa ya Mwanza,Simiyu,Shinyanga mikoa mingine Tabora,Geita na Singida na kwamba mipango ya kupeleka maji makao makuu ya Nchi Dodoma imeanza.

Amesema mradi huo wa maji ya ziwa unaongeza idadi ya Watu wanaopata maji safi na salama hapa Nchini kwa kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia za kumtuma ndoo mama.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Kishapu Boniphace Butondo amesema mradi wa maji ya ziwa victory ni mkombozi kwa wakazi wa Kishapu na kuishukuru serikali kwa mradi huo.

Mhandisi wa Ruwasa wilaya ya Kishapu amesema zadi ya Shilingi bilioni 2 nukta 8 zimetumika katika mradi huo na kuongeza kwamba awali wakazi wa kata hiyo walikabiliwa na shida ya maji safi na salama.

Akishkuru kwa niaba ya wanawake wa kata hiyo Bibi sayi sayi amesema kwa sasa ndoa zao zipo salama baada ya kupata maji kwani walikuwa wakitumia muda mwingi kusaka maji na kusababisha mgogoro kwenye ndoa

Mbunge wa Kishapu Boniphace Butondo ,akishuhudua  huduma ya maji safi na salama  wakati ,Injia wa Ruwasa mkoa wa Shinyanga akimtwisha maji mkazi wa kishapu ,









Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464