Viongozi wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga wakiingia katika kata ya Kitangili kuzungumza na wanawake
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Kikundi cha Wanawake na Samia Mkoani Shinyanga kimewakumbusha wanawake wa manispaa ya Shinyanga kutimiza majukumu yao ya Ndoa ili kupunguza migogoro mbalimbali ya kifamilia inayosababisha migogoro na watoto wa mitaani.
Hayo ameyasema katibu wa wanawake na Samia Mkoa wa ShinyangaTatu Juma Almasi wakati akiongea na wanawake wa kata ya Kitangili katika manispaa ya Shinyanga mkoani hapa kwa lengo la kutambulisha kikundi hicho na kufanya uchaguzi wa viongozi wa wanawake na Samia ngazi ya kata, ambapo katika kikao hicho walihudhulia wanawake zaidi ya 300
Tatu amesema baadhi ya wanawake wamesahau majukumu yao ya kufamilia wanaamka asubuhi na kukimbilia kwenye mikopo umiza na kausha damu na kurudi usiku na kuwasahau watoto,huku wanaume wakiendelea kulalamika kwamba hawapati haki yao ya unyumba.
"Kina mama wenzangu lengo kubwa la kuja hapa ni kuja kutambulisha kikundi chetu na kuelezea kazi tunayofanya, ambacho kimeanzishwa kwa lengo la kuwakusanya wanawake wawe pamoja,kuwajengea uwezo na kuwapa elimu ili kutambua kazi zinazofanywa na Rais wetu mama Samia Suluhu na kumuunga mkono kwa kazi kubwa anazofanya "amesema Tatu .
"Pia mama yetu mama Samia anatukumbusha sisi wanawake tutimize majukumu yetu vizuri ili familia zetu ziwe salama,kwani wanaume wengi wanatulalamikia kwamba tumesahau majukumu yetu kutokana na ubize kwenye harakati za kutafuta fedha hali amvayo tumekuwa tukisababisha migogoro mingi kwenye ndoa zetu na kusababisha watoto wetu wanakuwa watoto wa mitaani, kubakwa na kulawitiwa, hivyo tubadilike tutimize wajibu wetu,"ameongeza Tatu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga Husna Ally amewaomba wanawake hao kujiunga na kikundi cha wanawake na Samia ili kuwa wamoja katika kumuunga mkono Rais kwa kazi anazozifanya, kwani wakiungana, ambapo pia aliwaomba wanawake wajiandikishe kwenye daftari la kudumu ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
"Nawakaribisha sana wanawake wenzangu tujiunge kwenye kikundi chetu cha wanawake na Samia ili tuendelee kumuunga mkono mama yetu mama Samia, na niwaombe tuhamasishe wanawake wenzetu wachukue fomu za kugombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa, na anayejiona anaweza akachukue fomu, tuna pinga kusema adui wa mwanamke ni mwanamke ni mwanamke, sasa tunasema adui wa mwanamke ni mwanaume,"amesema Husna.
Naye mwenyekiti msaidizi wa mwanamke na Samia Mkoa wa Shinyanga Ester Shida Kika amesema Rais amefanya mambo makubwa, miundombinu ya barabara ilikuwa haipitiki amejenga madaraja kila sehemu, elimu bure, Zahanati zilikuwa chache wanawake walikuwa wakipata shida, kutembea umbali kufuata huduma na kuhatarisha maisha yao,lakini sasa wanapata huduma karibu.
"Mama yetu mama Samia anahamasisha kupanda miti kwa wingi na kuweka mazingira yetu vizuri,hivyo kila mmoja apande miti na kuweka mazingira yetu vizuri tukifanya hivyo tutaepuka magonjwa ya milipuko niwaombe wanawake tupambane tuungane kwa pamoja ili kuhakikisha serikali inatimiza kazi zake i ,amesema Ester Kika.
Baada ya kutambulisha kikundi hicho walifanya uchaguzi wa kuchagua viongozi wa wanawake na Samia kata ya Kitangili ambapo amechaguliwa Catherine Mbelele kuwa mwenyekiti, Agnes Venas mwenyekiti msaidizi, Anastazia Manota katibu, Maria Juma katibu msaidizi, Paulina Andrea mhasibu, Shoma Jilulu Hamasa
Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka amewahimiza wanawake wadumishe upendo wawe kitukimoja, na wazisemee kazi za mama Samia Suluhu, kwani toka aingie madarakani amefanya mambo makubwa Shinyanga na Taifa kwa ujumla.
Baadhi ya wanawake akiwemo Salome Petro wamefurahishwa na kuanzishwa kwa kikundi hicho kwani wanaamini kitasaidia kutaleta mafanikio kwa wanawake wa kata ya Kitangili na kuondoa kero mbalimbali zilizopo.
Viongozi wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga wakiingia katika kata ya Kitangili kuzungumza na wanawake
Viongozi wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga wakiingia katika kata ya Kitangili kuzungumza na wanawake
Mwenyekiti wa wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga Husna Ally akizungumza na wanawake wa kata ya kitangili

Katibu wa wanawake na Samia Mkoa wa ShinyangaTatu Juma Almasi akizungumza na wanawake wa kata ya Kitangili

Mwenyekiti msaidizi wa mwanamke na Samia Mkoa wa Shinyanga Ester Shida Kika akizungumza na wanawake wa kata ya Kitangili

Katibu wa wanawake Samia wilaya ya Shinyanga ya Shinyanga mjini Sada Hamis akizungumza
Viongozi wa Wanawake na Samia wakifurahia
Viongozi wa Wanawake na Samia wakiwa kwenye kikao hicho Kitangili
Diwani wa kata ya Kitangili Mariam Nyangaka akizungumza na wanawake wa kata hiyo
Wanawake wa kata ya Kitangili wakiwa kwenye kikao cha Wanawake Samia katika kata ya Kitangili manispaa ya Shinyanga