Header Ads Widget

WATOTO WA KANISA LA PHILADELPHIA SHINYANGA MJINI WAWAKUMBUSHA WAZAZI KUWALEA WATOTO KATIKA MAADILI MEMA YA KIMUNGU

Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakiwa kwenye picha ya pamoja katika sherehe ya watoto


Suzy Butondo, Shinyanga press blog

Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample lililoko maeneo ya Ndembezi manispaa ya Shinyanga wamewaomba wazazi kuwalea watoto wao katika maadili mema ya kimungu na kuzungumza naomara kwa mara, ikiwa ni pamoja na kuwahimiza kwenda kanisani kupata mafundisho ya neno la Mungu

Hayo wameyasema hivi karibuni kwenye sherehe yao iliyofanyika katika kanisa hilo, ambapo waliwaomba wazazi kuwalea malezi mema ya kimungu, ili wasijiingize kwenye makundi mabaya 

Dainess Ditrick akisoma risala kwa niaba ya watoto wa kanisa hilo alisema wazazi wengi wamekuwa hawatekelezi wajibu wao wa kuwafundisha maadili mema watoto wao kwa kuwa bize na shughuli zao, hivyo wameomba wawakumbuke, katika kuzungumza nao na kuwaonyesha upendo wanaporudi kutoka kwenye shughuli zao

"Tunawaomba wazazi wetu muendelee kuwa karibu nasi tunapokosea mturudishe kwenye msitari ili tusijiingize kwenye vitendo vya uovu visivyompendeza Mungu, msiwe bize na majukumu yenu mkatusahau, watoto wengi wanakuwa na tabia mbaya,na wengine kuwa watoto wa mitaani kutokana na kukosa malezi bora kwa wazazi wao"alisema Dainess.

Kwa upande wake mchungaji kiongozi wa kanisa hilo Baraka Laizer aliwapongeza kwa kufanikisha sherehe yao kwa wakati, ambapo aliwahimiza waendelee kujifunza neno la Mungu na kuwa na maadili mema. katika jamii

"Ujumbe uliotolewa na watoto hawa ni ujumbe mkubwa sana na ni wa muhimu sana kwa wazazi wote, hivyo tumekumbushwa kuwafundisha watoto wetu maadili mema tunatakiwa tufanye hivyo ili waweze kukua huku wakimjua Mungu"alisema Laizer 
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakiwa kwenye picha ya pamoja katika sherehe ya watoto

Mchungaji kiongozi wa kanisa la Philadelphia miracle Tample Baraka Laizer akizungumza kwenye sherehe ya watoto ambapo aliwapongeza kwa kufanikisha kufanya sherehe yao kwa wakati na kuwataka waendelee kumjua Mungu siku zote za maisha yao
Mchungaji kiongozi wa kanisa la Philadelphia miracle Tample Laizer Baraka akiwa na mke wake Evaline Msangi kwenye sherehe ya watoto
Mchungaji kiongozi wa kanisa la Philadelphia miracle Tample Baraka Laizer akiwa na mke wake Evaline Msangi akipokea zawadi kutoka kwa watoto wa kanisa hilo katika siku ya sherehe ya watoto
Mchungaji Baraka Laizer akimpongeza mtoto ambaye alitaja vitabu vyote vya biblia bila kusoma
Wachungaji wasaidizi wa kanisa la Philadelphia Miacle Tample wakipewa zawadi na watoto wa kanisa hilo

Walimu wa watoto kanisa la Philadelphia Miacle Tample wakiwa kwenye picha ya pamoja
Wachungaji wasaidizi wa kanisa la Philadelphia wakiwa na wake zao baada ya kupokea zawadi kutoka kwa watoto

Dainess Ditrick akisoma risala ya watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample
Dainess Ditrick akisoma risala ya watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakimsifu Mungu kwenye sherehe yao
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakifanya maigizo
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakimwabudu Mungu
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakitaja maandiko na mistari ya biblia waliyokariri
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakifanya maigizo

Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakimwabudu Mungu
Watoto wa kanisa la Philadelphia Miracle Tample wakifanya maigizo
Walimu wa watoto wakipongezana kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kufundisha watoto

Post a Comment

0 Comments