Wanafunzi wa chuo cha Hill Forest wakiingia katika ukumbi wa sherehe ya mahafali ya 10
Suzy Butondo, Shinyanga press blog
Wazazi wenye watoto waliohitimu katika chuo cha Hill Forest kilichopo mjini Shinyanga wameishukuru serikali
kwa kuwafadhili watoto wao kwa kusoma bure katika chuo hicho, kwani elimu waliyoipata itawasaidia kuajiliwa na kujiajili wenyewe ili kujikwamua kiuchumi.
Shukurani hizo wamezitoa jana kwenye Mahafali ya kumi (10) katika chuo hicho ambapo wamehitimu wanafunzi 290, huku mgeni rasmi akiwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Ramadhan Masumbuko aliyekuwa amemwakilisha mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini ambaye pia ni Naibu Waziri kazi, vijana, ajira na wenye ulemavu
Katika mahafali hiyo ya 10 wamehitimu wanafunzi 290 wenye kozi mbalimbali zikiwemo kozi ndefu na kozi fupi wakiwemo watalamu wa ofisi za mapokezi (front office operation), Waalimu wa kufundisha shule ya Nassary pamoja na Wasaidizi wa Maabara
Wazazi hao wameishukuru serikali kwa kusaidia kuwasomesha bule watoto wao kwani baadhi yao walikuwa hawana uwezo wa kuwapeleka chuo, lakini kwa upendo wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan wameweza kusoma na wamehitimu vizuri.
"Tunaishukuru sana serikali yetu ya mama Samia pamoja na waziri mkuu Kassimu Majariwa bila kumsahau mbunge wetu Patrobas katambi kwa kushirikiana na viongozi hawa wa kitaifa kutusaidia kuwasomesha watoto wetu, hawa waliohitimu leo, tunaiomba serikali yetu tukufu iendelee kutukumbuka na kutusaidia zaidi, iendelee kutufadhili na awamu nyingine"amesema Juliana Thobias
"Mimi sina cha kusema zaidi namshukuru mama yetu mama Samia, waziri mkuu na mbunge wetu Patrobas Katambi, hivyo niwaombe watanzania wote tuungane kwa pamoja tuweze kuwaombea ili waendelee kutukumbuka na kuwakumbuka watoto wetu katika awamu nyingine na niwaombe watanzania na wanashinyanga tuwaunge mkono viongozi hawa ili waendelee kufanya maendeleo makubwa katika maeneo yetu mbalimbali"amesema Patrick Simon.
Wakizungumza baadhi ya wanafunzi ambao wamehitimu masomo yao akiwemo Johari Malunde wameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ufadhili huo, huku wakiahidi kutumia ujuzi huo kwenda kuleta mabadiliko chanya katika jamii na taifa kwa ujumla.
"Tunaishukuru sana serikali ya mama Samia Suluhu kwa kutupatia ufadhili huu ambapo tayari tumechukua ujuzi, hivyo kutokana na maadili mazuri tuliyofundishwa katika chuo hiki tunaamini tutafanya vizuri , kokote tutakapoajiliwa na kujiajiri"amesema Malunde.
Akizungumza katika mahafali hayo, kwa njia ya simu Mbunge wa jimbo la Shinyanga Katambi amesema serikali inaendelea kuweka mazingira rafiki kuhakikisha vijana wote wanaopata mafunzo kwenye vyuo wanapata vifaa ama mikopo ili kuendeleza ujuzi wao huku akiwasisitiza kutokukata tamaa.
“Nawapenda sana wapenda sana na nawaahidi kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila mmoja wetu ananufaika na Shinyanga yetu katika uwekezaji na kuleta maendeleo kwenye sekta zote za elimu, miundombinu, sekta ya Afya, sekta ya Kilimo na sekta zingine zote zinazosababisha kuweza kuleta mzunguko wa fedha katika Manispaa yetu ya Shinyanga”.amesema Katambi.
“Niwaombe wazazi waendelee kutupa ushirikiano na wanafunzi wahitimu tuendelee kupambana tuhakikishe kwamba elimu hiyo tuliyoipata itusaidie zaidi katika kuweza kuinua uchumi wetu binafsi, lakini pia wa familia zetu na kushiriki katika ujenzi wa taifa”.amesema Katambi
“Kuna mifumo ya mikopo ipo tutaendelea kuhakikisha kwamba wale wahitimu basi tunawawezesha kama siyo mikopo basi vifaa ili waweze kufanya kazi na kuitumia elimu hiyo kwa ajili ya ujenzi wa taifa kikubwa msikate tamaa, tufanye kazi, tupambane usiku na mchana tunachotakiwa usihame kwenye malengo yako, achana na wale wanaokusema vibaya kukukatisha tamaa wewe angalia mbele hakika utafanikiwa na sisi tunawaahidi kuwatengenezea mazingira wezeshi”.aliongeza Katambi.
Kwa upande wake Mgeni rasmi, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko amewataka wakazi wa Manispaa hiyo kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali zikiwemo fursa katika sekta ya elimu ili kupata elimu na ujuzi ambao utasaidia kujikwamua kiuchumi.
“Serikali imeweka utaratibu wa fursa mbalimbali ambazo vijana wetu wakiweza kuzitumia wataingia kwenye ajira zao binafsi na wanaweza kurejesha fedha ya serikali,lakini pia wao wenyewe watatengeneza ajira kwa watu wengine na ndiyo lengo la serikali, kwahiyo nianze kwa kuwapongeza vinaja ambao mmehitimu mafunzo yenu nina amini mtakwenda kuyasimamia maadili yote mliyopewa hapa shuleni ili kuwa faida kwenu na faida kwa taifa,"amesema Masumbuko.
"Pia niwaombe mdumishe nidhamu na kuyalinda maadili, mtambue kuwa hakuna mwajiri ambaye anaweza kukaa na mfanyakazi wake ambaye hafanyi kazi kwa juhudi, lakini pia niwaombe vijana tuchangamkia fursa hasa za kielimu katika Manispaa yetu ya Shinyanga kuliko kukaa nyumbani na wengine kujihusisha kwenye makundi mabaya kama uvutaji sigara, pombe na wengine kucheza michezo ya kubahatisha”.ameongeza Masumbuko.
Kwa upande wake mkurugenzi wa chuo cha Hill Forest Shinyanga John Siagi amemshukuru mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini Katambi kwa kutoa ushirikiano mkubwa na juhudi alizozifanya katika kufanikisha ufadhili huo kwa wanafunzi 290, Mungu ambariki.
Aidha amewakumbusha wazazi na walezi ambao wanaishi na watoto nyumbani kuhakikisha wanachangamkia fursa hizo zinazotolewa na serikali ili watoto waweze kujiendeleza na kujikwamua kiuchumi.
“Niwaombeni wazazi wenzagu kama tuna watoto wako nyumbani tutumie fursa hizo na ukweli sisi Shinyanga bado tumelala tuamke, watoto tusiwaache wakazagaa majumbani na mitaani tunafursa hizo na kwa bahati nzuri hujachelewa bado wapo wanafunzi watakao ingia hapa awamu nyingine ambayo tunaanza kupokea wanafunzi mwezi wa tisa hivyo tunawakaribisha mwezi wa tisa siyo mbali ni kipindi kizuri kufanya maadalizi,amesema Siagi.
Naye diwani viti maalum Zuhura Waziri aliwasihi wanafunzi hao waliohitimu wakawe na maadili mema wasijiingize kwenye makundi yasiyofaa badala yake wakawe mabalozi wazuri na wakamsemee vizuri Rais Samia kwa kazi anazozifanya, na wakaepuke tamaa ndogo bdogo wasitake mafanikio ya haraka wakawe wavumilivu.
Aidha katika taarifa yake mkuu wa chuo cha Hill Forest Shinyanga, Fortunata Paschal Shine ameeleza mambo mbalimbali ikiwemo mafanikio ya chuo hicho huku akiishukuru na kuipongeza serikali kwa kuendelea kutoa fursa kwa vijana.
“Chuo chetu hiki kilianzishwa mwaka 2012 enzi hizo kikiwa na kozi mbili ambazo ni wasaidizi wa maabara na watalamu wa ofisi za mapokezi yaani "front office operation, kutokana na uzoefu tulioendelea kuupata toka chuo kimeanzishwa tumeweza pia kuongeza kozi fupi na ndefu ikiwa pamoja na Ualimu wa watoto wadogo, habari na mawasiliano pamoja na mapishi, chuo chetu hapo awali kilikuwa na vyumba viwili vya madarasa na watumishi wasiopungua wanne”.
“Chuo chetu kimesajiliwa na kutamburika na serikali kikiwa chini ya NACTIVET, napenda kutoa shukrani kwa niaba ya uongozi mzima wa chuo chetu, shukran ziende kwa serikali ya jamhuri ya muongano ya Tanzania china ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na wasidizi wake wote kwa kutupa kipaumbele na kuamini juu ya fursa hii adimu sana ya mpango wa maendeleo na kukuza ujuzi kwa vijana wa kitanzania, hakika tumeiona ni njema serikili yetu kwa kuwajengea uwezo vijana wetu wa kuajiliwa na kujiali wenyewe"amesema Fortunata.
“Lakini nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipo kushukuru mbunge wa jimbo la Shinyanga, kwa jitihada kubwa unazo endelea kizifanya za kuwatetea,kuwapambania na kuwawezesha vijana wengi ndani ya jimbo la Shinyanga mjini na maeneo jirani, napenda kuwajulisha vijana wetu wanao hitimu leo pamoja na wazazi waliopo ya kwamba,bila katambi fursa hii huenda tungeikosa,tunakushukuru sana”.ameongeza.
“Mafanikio tulio yapata hadi sasa hasa baada ya kupata fursa ya mpango huu wa ukuzaji wa ujuzi ambao umefadhiliwa na serikali kwa asilimia mia moja ya ada ya mafunzo, tumeongeza vyumba vya madarasa hadi kufikia vinane, tumeongeza walimu hadi kufikia 11 pamoja na watumishi wasio kuwa waalimu 9,aidha tumeongeza ofisi hadi kufikia 14, tumefanikiwa kuwa na mradi wa maji ya kisima na kuwa na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa matumizi ya wana chuo na kilimo cha mboga mboga na matunda" amesema Fortunata
"Matarajio ya chuo chetu ni makubwa sana kifupi tunataraji kuwa kituo bora cha mwanzo wa maarifa na ujuzi kwa kusudio la kudahili hadi kufikia wanachuo kwa maelfu,kukuza kipato na kuongenza huduma kwa jamii na kushiriki kikamilifu katika harakati za kuipunguzia mzigo serikali juu ya fursa za ajira kwa vijana wa kitanzania.
Fortunata ameiomba serikali iendelee na moyo huo wa dhati wa kuwafadhiri watoto hasa ambao hawana uwezo na wale ambao wamekosa nafasi ya kuendelea na masamo kutokana na sababu mbali mbali ili kuwasaidia wazazi na vijana wenyewe.
"Chuo hiki kinauwezo kina uwezo wa kudahiri zaidi ya wanachuo 600 kwa mwaka, vile vile tuwaombe wazazi waendelee kukiamini na kushiriki kukijenga chuo chetu kwa kutuletea vijana ili nia yetu njema tunayo ionyesha kwa utekelezaji iweze kuzaa matunda tunayo yatamani.”amesema Fortunata
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mahafali ya 10 katika cha Hill Forest
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mahafali ya 10 katika cha Hill Forest
Mstahiki Meya wa manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akizungumza kwenye mahafali ya 10 katika cha Hill Forest
Mkurugenzi wa chuo chaHill Fores John Siagi akizungumza kwenye mahafali ya 10
Mwenyekiti ws bodi ya chuo hicho mchungaji Daniel Manga akizungumza
Wanafunzi wa kozi ndefu wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na viongozi wa chuo hicho
Wanafunzi wa kozi fupi wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na viongozi wa chuo hicho
Wanafunzi wa kozi fupi wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na viongozi wa chuo hicho
Wahitimu wakimkabidhi Keki mkurugenzi wa chuo hicho John Siagi
Wanafunzi wa chuo wakipokea vyeti
Wanafunzi wa chuo wakipokea vyeti
Wanafunzi wa chuo wakipokea vyeti
Wahitimu
Wanafunzi wa chuo hicho wakisoma risala
Wanafunzi wa chuo cha Hill Forest wakiingia katika ukumbi wa sherehe ya mahafali ya 10
Wanafunzi wa chuo cha Hill Forest wakiingia katika ukumbi wa sherehe ya mahafali ya 10
Wanafunzi wa chuo cha Hill Forest wakiingia katika ukumbi wa sherehe ya mahafali ya 10
Wanafunzi wakipokea vyeti
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464