Na Mwandishi wetu Shinyanga press blog
Zaidi ya wakazi 15,000 katika kata ya Uchunga wilayani Kishapu mkoani Shinyanga wameanza kunufaika na maji ya ziwa victory ambapo imesaidia kuondoa migogoro katika ndoa.
Mmoja ya wakazi wa kata hiyo sayi sayi amemwambia naibu waziri wa maji mhandisi Methew Kundo alipotembelea mradi huo, kwamba wanashukuru sana kwa kupatiwa maji safi na salama kwani walokuwa wakipata shida kufuata mbali na wakati mwingine kusababisha migogoro ya ndoa.
Sayi amesema walikuwa wakiamka usiku wa manane kutafuta maji na kuwaacha waume zao wamelala jambo ambalo lilisababisha migogoro kwenye familia zao na wengine kupigwa.
Amesema kwa sasa migogoro imeondoka hivyo ameipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri, ya kuwapelekea maji ya ziwa Victoria.
Awali mbunge wa jimbo la Kishapu Boniface Butondo alisema mradi huo umegharimu zaidi ya bilioni 2.8 na kuongeza kwamba Serikali imefanya kazi kubwa.
"Niwaombe tu wanakishapu wote ambao hawajafikiwa na mradi wa maji haya ya Ziwa Victoria tuendelee kuvumilia, kwani serikali inampango wa kufikisha maji haya kila kijiji,"amesema Butondo
Kwa upande wake naibu waziri wa maji Kundo amesema Serikali inaendelea kujenga miradi ya maji katika wilaya ya Kishapu, hivyo wanakishapu wote watafikiwa na maji hayo awamu kwa awamu