Header Ads Widget

BALOZI WA SWEDEN NCHINI TANZANIA ATEMBELEA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA KILIMANJARO

 

Balozi wa sweeden,Uongozi wa UTPC na wanachama wa MECKI katika picha ya pamoja baada ya kikao.
Balozi wa Sweeden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias akisaini kitabu cha wageni ofisi ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanjaro.

Na mwandishi wetu.

 Balozi wa Sweden nchini Tanzania Mh. Charlotta Ozaki Macias  ametembelea Klabu ya waandishi wa Habari Kilimanjaro (MECKI) kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na klabu hiyo pamoja na kufanya mazungumzo na wanachama wa mkoa huo.

Mh. Balozi huyo pia ametaka kujua mchango wa MECKI kwa jamii katika kupaza sauti ili kuibua changamoto zilizopo kwenye jamii na namna klabu hiyo ilivyojipanga kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu na uchaguzi mkuu wa 2025. Ziara ya balozi huyo ilifanyika jana agosti 5,2024.

Pamoja na mambo mengine Mhe  Balozi na wanachama hao wamejadiliana masuala mbalimbali  ikiwemo uhuru wa vyombo vya habari na namna ya kuandika habari za uchaguzi.

Aidha Mhe. Charlotta ameambatana na timu kutoka Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) iliyokuwa ikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji  Kenneth Simbaye.

Balozi wa Sweeden akizumgumza na wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Kilimanjaro katika ziara ya kufahamu maendeleo ya klabu hiyo.




Wanachama wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanjaro wakisikiliza mazungumzo ya balozi wa Sweden -chini Tanzania.

Balozi wa sweden akiwaga viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanjaro.

Post a Comment

0 Comments