KESI YA SEPTEMBA 11KUNGURUMA WIKI IJAYO


Kesi ya Septemba 11 kunguruma wiki ijayo
Na Kulthum AllyAugust 1, 2024

MAREKANI: Wanaume watatu wanaotuhumiwa kupanga mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 wamekubaliana na upande wa mashtaka kabla ya kesi yao kuanza kusikilizwa

Makubaliano hayo ni kwamba wanatakiwa kukubali wanahatia ili upande wa mashtaka usiombe hukumu ya kifo.

Mpaka sasa watu ambao wamezuiliwa katika kambi ya Jeshi la Wanamaji la Marekani Guantanamo Bay, Cuba, kwa miaka mingi bila kufikishwa mahakamani ni Khalid Sheikh Mohammad, Walid Muhammad Salih Mubarak Bin Attash, na Mustafa Ahmed Adam al-Hawsawi

Takriban watu 3,000 huko New York, Virginia na Pennsylvania waliuawa katika mashambulizi ya al-Qaeda, ambayo yalisababisha Vita dhidi ya Ugaidi na uvamizi wa Afghanistan na Iraq.

Mpango huo ulitangazwa kwa mara ya kwanza katika barua iliyotumwa na waendesha mashtaka kwa familia ya waathiriwa.

Hili lilikuwa shambulio baya zaidi kwenye ardhi ya Marekani tangu shambulio la mwaka 1941 la Japani kwenye Bandari ya Pearl, Hawaii, ambapo watu 2,400 waliuawa.

“Kwa makubaliano ya kuondolewa kwa adhabu ya kifo kama adhabu inayowezekana kutolewa, washtakiwa hawa watatu wamekubali kukiri makosa yote yaliyokuwa yakishitakiwa likiwemo la mauaji ya watu 2,976 waliotajwa kwenye hati ya mashtaka,”aliandika mwendesha mashta

Soma hapa zaidi chanzo habari leo
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464