Butondo aongoza harambee ya ujenzi wa Kanisa KKKT Mwamalasa, Shilingi Milioni 10 zapatikana
Na Mwandishi wetu,KISHAPU
MBUNGE wa Jimbo la Kishapu Boniphace Butondo, ameongoza harambee ya ujenzi wa kanisa la KKKT Mwamalasa katika wilaya hiyo, ambapo kiasi cha Shilingi milioni 10 kimekusanywa.
Harambee hiyo imefanyika leo, Agosti 3, 2024, na kuhudhuliwa na waumini wa kanisa hilo pamoja na wadau wa maendeleo.
Katika harambee hiyo Mbunge Butondo amechangia kiasi cha fedha Shilingi milioni 2, huku Askofu Dk. Yohana Nzelu wa KKKT Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria akichangia Shilingi milioni 4.
Akizungumza kwenye harambee hiyo, amesema wao kama viongozi wanatambua mchango mkubwa ambao unafanywa na viongozi wa dini, katika kuiombea amani nchi,pamoja na kuwafanya wananchi wawe na hofu ya mungu na hatimaye kuishi wa amani,upendo na utulivu.
Amelipongeza pia Kanisa hilo la KKKT kwa kuendelea kusambaza kuhuduma za kidini hadi maeneo ya vijijini, na kwamba wataendelea kuwaunga mkono.
"Nawashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuiombea amani nchi yetu, pamoja afya njema mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuwatumikia Tanzania na kuwaletea maendeleo na sisi kama viongozi tutaendelea kuwaunga mkono," amesema Butondo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464