Header Ads Widget

WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUPITIA RUWASA KUWATEKELEZEA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA


WANANCHI WAISHUKURU SERIKALI KUPITIA RUWASA KUWATEKELEZEA MRADI WA MAJISAFI NA SALAMA

Na Marco Maduhu,KAHAMA
WANANCHI wa vijiji vya Chona,Bukomela na Ubagwe halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama,wameishukuru Serikali kupitia wakala wa maji vijijini (RUWASA)kwa kuwatekelezea mradi wa majisafi na salama.

Wamebainisha hayo leo Agosti 14,2024 wakati Mwenge wa uhuru ulipowasili kuweka jiwe la msingi, kwenye ujenzi wa mradi huo katika Tenki la maji lililopo kijiji cha Chona.
Mmoja wa wananchi hao Neema Selemani,amesema wamekuwa wakipata shida kutafuta maji safi na salama umbali mrefu,pamoja na kuamuka majira ya usiku lakini mradi huo ukikamilika shida hiyo haitakuwepo tena.

"Mradi huu wa maji utakapokamilika, utatusaidia sisi wananchi hasa wanawake kuondokana na adha ya kufuata maji umbali mrefu, amesema Neema.
Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava, amewapongeza RUWASA kwa utekelezaji wa mradi huo wa maji, pamoja na kufuata taratibu za utangazaji zabuni kwa kutumia mfumo wa mtandao NeST.

"Madhumuni ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi katika maeneo yote wanapata huduma ya majisafi na salama, na ndiyo maana amekuwa wakiidhinisha fedha na kutekelezwa miradi ya maji na kumtua ndoo kichwani mwanamke,"amesema Mnzava.
"Mradi huu ni wa kisima kirefu, hivyo natoa wito kwa wananchi muendelee kutunza vyanzo vya maji ili kuwepo na uhakika wa maji, na kuendelea kutekelezewa miradi kama hii na kuwaondolea adha ya ukosefu wa majisafi na salama katika maeneo yenu," ameongeza.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani, amewapongeza RUWASA kwa usimamizi mzuri wa mradi huo, ambao utamaliza tatizo la ukosefu wa majisafi na salama kwa wananchi katika vijiji hivyo.
Meneja wakala wa maji vijijini (RUWASA)wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili,awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji, amesema Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mpango wake wa kumtua ndoo kichwani mwanamke, walipata fedha kupitia mpango wa malipo kwa matokeo kiasi cha Sh.bilioni 1.4 ili kutekeleza mradi huo.

"Wananchi wa vijiji vya Chona,Bukomela na Ubagwe ni miongoni mwa vijiji ambavyo vinashida ya maji,na ujenzi wa mradi huu utakapokamilika utamaliza changamoto hiyo ya ukosefu wa huduma ya majisafi na salama,"amesema Mhandisi Magili.
"Mradi huu ulianza rasmi kutekelezwa 14,2,2024 na unatarajiwa kukamilika Novemba11 mwaka huu,na wananchi 5,763 watanufaika kwa kupata huduma ya majisafi na salama," ameongeza.

Aidha,amesema mradi huo utekelezaji wake hadi sasa umefikia asilimia 55 chini ya Mkandarasi kutoka Kampuni ya Jonta Investment Limited.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava (kushoto) akikata utepe kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi mradi huo wa maji katikaTenki la maji lililopo kijiji cha Chona,(kulia) ni Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava (kushoto) akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa maji katikaTenki la maji lililopo kijiji cha Chona,(kulia) ni Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Mnzava (kushoto) akiweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa mradi wa maji katikaTenki la maji lililopo kijiji cha Chona,(kulia) ni Mbunge wa Ushetu Emmanuel Cherehani.
Awali Meneja wa Ruwasa wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akielezea ujenzi wa mradi huo wa maji.
Tenki la maji ambalo lipo katika kijiji cha Chona.
Mwenge wa uhuru ukiwa katika Tenki la maji katika kijiji cha Chona

Post a Comment

0 Comments