Header Ads Widget

MWENGE WAZINDUA UPANUZI MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA ZONGOMERA-NYANDEKWA WANANCHI 9,268 WAMENUFAIKA


MWENGE WAZINDUA UPANUZI MRADI WA MAJI ZIWA VICTORIA ZONGOMERA-NYANDEKWA WANANCHI 9,268 WAMENUFAIKA

Na Marco Maduhu,KAHAMA
MWENGE wa uhuru umezindua upanuzi wa mradi wa maji kutoka Zongomera hadi Nyandekwa halmashauri ya Manispaa ya Kahama,na kuwaondolea adha wananchi ya ukosefu wa majisafi na salama.

Uzinduzi huo umefanyika leo Agosti 15,2024 katika kijiji cha Nyandekwa.
Meneja wakala wa maji vijijni (RUWASA)wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili,akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo,amesema wameutekeleza kwa kushirikiana na Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Kahama (KUWASA)na sasa upo chini ya Kuwasa.

Amesema mradi huo ulianza kutekelezwa februari 2022,na kukamilika januari 2024, na umewafikia wananchi 9,268 kati ya 16,375 wa Kata ya Nyandekwa, kutoka katika vijiji vya Lowa,Buduba,Bujika na Nyandekwa.
"Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Mheshimiwa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha za mradi huu Sh.bilioni 1.4,"amesema Mhandisi Magili.

Naye kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kiraifa Godfrey Mnzava, akizungumza mara baada ya kuzindua mradi huo, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya mradi huo.
Nao baadhi ya wananchi wa Nyandekwa wameshukuru kwa mradi huo wa maji,na kwamba sasa hivi wanatumia majisafi na salama.

Mwenge wa uhuru katika manispaa ya Shinyanga unakimbizwa umbali wa kilomita 64.8 na kumulika miradi 8 ya maendeleo yenye thamani ya sh.bilioni 13.9.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu 2024, inasema"Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu".
Meneja wa RUWASA wilaya ya Kahama Mhandisi Maduhu Magili akielezea upanuzi wa mradi huo kutoka Zongomera hadi Nyandekwa.
Mwenge wa uhuru.

Post a Comment

0 Comments