Header Ads Widget

VIFO VYA MIFUGO TISHIO WILAYANI SHINYANGA

VIFO VYA MIFUGO TISHIO WILAYANI SHINYANGA

Na Marco Maduhu,SHINYANGA
HALMASHAURI ya wilaya ya Shinyanga wamelalamikia kukithiri kwa vifo vya mifugo,hali ambayo inatishia kushuka kwa uchumi wa familia za wafugaji na taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 20,2024 kwenye kikao cha baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza kwenye baraza hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Ngassa Mboje,amesema hali ni mbaya wilayani humo juu ya kukithiri kwa vifo vya mifugo, na hivyo kuiomba Serikali kupitia wizara ya mifugo iingilie kati ili kunusuru tatizo hilo.

“hali ni mbaya ya vifo vya mifugo wilayani Shinyanga, mimi mwenyewe nina ng’ombe 100 lakini nusu yake wote wamekufa, na wananchi kila siku wanalia mifugo kufa na hatujui ni ugonjwa gani, na imani imeanza kuzagaa huenda chanjo ya mifugo ndiyo tatizo,tunaomba Serikali itunusuru kwa hili,”amesema Mboje.
Mbunge wa Vitimaalumu Christina Mzava.

“Uchumi wa wananchi wetu unategemea kilimo na mifugo, hivyo mifugo inavyokufa na uchumi wa taifa letu unatoweka, wizara ya mifugo tunaomba ituangalie hapa wilaya ya Shinyanga,” ameongeza.

Afisa kilimo,mifugo na uvuvi halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Edward Maduhu, amekiri mifugo wilayani humo inakufa na bado hana takwimu sahihi, na kwamba sasa wapo kwenye utaratibu wa kuanzisha maabara yao, ili kufanya uchunguzi wa kubaini ugonjwa ambao unasababisha mifugo hiyo kufa, na pia wameshatoa taarifa kwa waratibu wa magonjwa ya mifugo kanda ambao wapo jijini Mwanza.
Nao baadhi ya wafugaji wilayani Shinyanga wamelalamikia kukithiri kwa vifo vya mifugo yao, na kuiomba Serikali iwanusuru sababu baadhi yao wamesharudi nyuma kiuchumi na hawana mifugo kabisa yote imekufa.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI👇👇
Kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kikiendelea.
Kikao cha baraza la madiwani wilayani Shinyanga kikiendelea.

Post a Comment

0 Comments