Header Ads Widget

KAMPENI YA MSAADA WA KISHERIA YA MAMA SAMIA YATOA HUDUMA MAONESHO YA NANE NANE DODOMA

Kampeni ya Msaada wa kisheria ya Mama Samia yazidi kutoa huduma katika maonesho ya nanenane Dodoma

Na Mwandishi Wetu

BAADA ya kusaidia maelefu ya Watanzania kupitia Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF), Kampeni ya Kitaifa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia, maarufu kama Mama Samia Legal Aid Campaign, sasa iko katika maonesho ya Nanenane jijini Dodoma.

Kampeni hiyo, iliyozinduliwa mwaka jana, imekuwa ikitumia wabobezi wa sheria kutatua migogoro mbalimbali katika mikoa wanayopita. Katika maonesho haya, inatoa msaada wa kisheria kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na elimu kuhusu haki za kisheria na jinsi ya kuzitafuta.

Mama Samia Legal Aid Campaign inatoa fursa kwa wananchi kukutana na wataalamu wa sheria bila gharama yoyote, wakishughulikia masuala kama vile kifamilia, mirathi, na mengineyo. Kampeni hii, inayotarajiwa kuendelea hadi Februari 2026, tayari imewafikia zaidi ya watu 500,000 katika mikoa saba: Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu, Manyara, Njombe, na Ruvuma.

Post a Comment

0 Comments