DC MKUDE: MICHEZO NI NJIA MUHIMU YA KUIMARISHA AFYA NA MSHIKAMANO KATIKA JAMII

Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Joseph Mkude,ameihasa jamii kupenda michezo sababu ina imarisha na kujenga mshikamano katika jamii.

Amebainisha hayo jana alipokuwa mgeni Rasmi katika fainali ya Salumu Cup iliyofanyika katika viwanja vya Badi Kata ya Mwakipoya.

Fainali hiyo ilikutanisha timu mbili, Gazza FC kutoka Kishapu na Sanga Itinje FC kutoka Meatu, ambapo Gazza FC ilishinda kwa magoli 2-0.

Amesema anazipongeza timu zote zilizoshiriki mashindano hayo,huku akisisitiza kuwa michezo ni njia muhimu ya kuimarisha afya na kujenga mshikamo katika jamii.

Aidha,ametoa wito kwa wananchi kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye daftari la kudumu la wapiga kura,zoezi litakalo anza tarehe 21-27 Agosti 2024, pamoja na kujitayarisha kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Naye Mbunge Kisesa, Mhe. Luhaga Mpina, amezipongeza timu zote kwa mchezo mzuri na kuahidi kuendelea kuunga mkono vijana katika masuala ya michezo.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464