Header Ads Widget

MIILI YA WATU WATATU YAFUKULIWA KWA MGANGA


Kesi ya watu kuripotiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha mkoani Singida imeendelea kuchukua sura mpya baada ya miili ya watu watatu kuripotiwa kuuwawa kwa imani za kishirikina.
Jeshi la Polisi limetoa mwendelezo wa taarifa yake iliyotolewa Agosti 24 mwaka huu ya kukamatwa kwa watu watatu ambao ni Selemani Nyandalu, Saidi Haji na Nkamba Kasubi ambae ni mganga wa kienyeji waliohusishwa katika mauaji hayo.

Watu hao wamelionyesha Jeshi la polisi mahali walipo wafukia watu hao akiwemo Samwaja Sifaeli Saidi ambae walimuuwa na kukata sehemu zake za siri.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imeeleza Agosti 24, 2024 mashimo mawili yalibainika ambapo baada ya kufukuliwa ulipatikana mwili wa Gideon Samweli mkazi wa makuro mkoa wa singida ambae mara ya mwisho alionekana amepakiwa kwenye pikipiki Octoba 15 2023, na taarifa za kutoweka kwake kurIpotiwa polisi na mwili mwingine uliokuwa haujatambulika ila ni mabaki ya mwili huo.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO EATV

Post a Comment

0 Comments