SHY EVAWC WATAKA BINTI ALIYEFANYIWA UKATILI APATIWE MSAADA WA KISAIKOLOJIA,WAKITOA TAMKO KULAANI TUKIO HILO
KIKUNDI kazi cha kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga (Shinyanga EVAWC Working Group) kimetoa tamko la kulaani kitendo cha kikatili alichofanyiwa binti cha kubakwa na kulawitiwa (jina limehifadhiwa) mkazi wa Temeke Dar es salaam,na vijana watano wanaodaiwa kuwa wanajeshi, na kisha kumrekodi video na kusazambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii,huku wakitaka binti huyo apatiwa msaada wa kisaikolojia.
Tamko hilo limetolewa leo Agosti 7,2024 na kwa waandishi wa habari na mwanachama wa kikundi hicho Anascholastika Ndangiwe kwa niaba yao, ambaye pia ni Mwenyekiti wa taasisi ya wanawake laki moja.
Amesema kwa kauli moja wanalaani kitendo hicho cha kikatili alichofanyiwa binti huyo, ambacho ni kinyume na sheria za nchi kupitia sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyorekebishwa mwaka 2022 inayoainisha makosa ya kingono, na kuomba adhabu kali ichukuliwe kwa mujibu wa sheria dhidi ya vijana hao.
“Shinyanga EVAWC Working Group kwa umoja wetu tunalaani vikali kitendo hiki kwani ni kinyume na sheria za nchi, na kwa mujibu wa sheria makosa ya kingono kama haya adhabu yake ni kifungo cha maisha au kisichopungua miaka 30 kulingana na mazingira ya kosa hilo, tunaviomba vyombo vya sheria zitoe adhabu kali dhidi ya vijana hawa watano waliomfanyia ukatili binti huyo,”amesema Ndagiwe.
“Pia tunakemea na kupinga vikali picha na video hizo za ngono kuendelea kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii sababu zinazidi kumfedhehesha binti huyo, na usambazaji wa video hizo ni ukiukwaji wa sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015.
Aidha, wametoa rai kwa taasisi zote zinazojihusisha na utoaji wa huduma za msaada wa kisaikolojia na huduma zingine za kibinadamu kuona namna wanavyoweza kuhakikisha binti huyo anasaidiwa ili awe sawa baada ya madhila yaliyompata.
“Tunasema haya sababu katika mijadala na yote na matamko rasmi ya mamlaka za serikali yanayotolewa tangu kuanza kwa sakata hili hatujasikia namna ambavyo binti huyu amepatiwa huduma ya kisaikolijia na huduma zingine kama miongozo ya utoaji huduma kwa madhura wa vitendo vya ukatili inavyoelekeza,”amesema Ndangiwe.
Aidha tukio hilo la kubakwa na kulawiti wa binti huyo jina limhifadhiwa mkazi wa Dar es salaam lilitokea Agost 3,2024 wakihusisha vijana watoto ambao ni wanajeshi kumfanyia tukio hilo la kinyama huku wakimrekodi video, na sasa vijana hao wametiwa nguvuni.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464