NDALICHAKO AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UALIMU NA UAMUZI WA MPIRA WA MIKONO

NDALICHAKO AFUNGA MAFUNZO YA AWALI YA UALIMU NA UAMUZI WA MPIRA WA MIKONO

Na. Paul Kasembo, SHY RS.

Katibu Tawala Msaidizi, Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mkoa wa Shinyanga Mwl. Dafroza Ndalichako amefunga mafunzo ya awali ya ualimu na uamuzi wa mpira wa mikono huku akiwataka wahitimu kwenda kuwa chachu katika kuibua vipaji vya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari,katika kuendeleza suala zima la michezo kwani sekta hii kwa sasa imekuwa ikizalisha ajira nyingi.

Ndalichako ameyasema wakati akifunga mafunzo ya awali ya waamuzi na walimu wa mpira wa mikono na marekebisho ya sheria za mpira wa mikono (HANDBALL) kwa shule za msingi na sekondari hapa katika shule ya sekondari Uhuru yenye lengo la kujifunza mabadiliko ya sheria ya mchezo huo yaliyofanyika tarehe 21 March 2024.

"Pamoja na kuwapongeza sana kwa kuhitimu mafunzo haya, lakini niwatake sasa kwenda kuwa chachu kubwa sana katika kuibua vipaji vya aanafunzi mashuleni kwenu ili tuweze kuwa na vijaba weye uwezo mkubwa katika mchezo huu ukizingatia kuwa kwa sasa michezo ni ajira kubwa sana," amesema Dafroza.

Kwa upande wake mkufunzi wa mafunzo haya kutoka Chama cha Mpira wa Mikono Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Ufundi Tanzania ndg. Emmanuel Majura amewaasa walimu waliopatiwa mafunzo haya kwenda kuyafanyia kazi kwa kuwafundisha wanafunzi katika vituo vyao vya kazi ili rasimali fedha iliyogharimia mafunzo haya iwe na tija kwa kuonekana kwa vitendo zaidi.

Awali akielezea matarajio ya baadae yatakayotokana na mafunzo haya Afisa Maendeleo ya Michezo Mkoa wa Shianyanga Bi. Jesca Simchile amesema ni kutengeneza timu za Mkoa wa Shinyanga zitakazocheza kwa weledi kuanzia ngazi ya Mkoa mpaka Taifa na kupelekea kupata wachezaji bora watakaoshiriki katika michuano ya mchezo huo kwa ngazi ya Afrika mashariki mwaka 2025.

Kando na viongozi hawa, walimu waliopatiwa mafunzo haya wametoa salamu za shukrani zaidi Chama cha Mpira wa Mikono katika Mkoa wa Shinyanga kwa kufanikisha upatikanaji wa elimu hii ,kwani itakwenda kuamsha ari ya michezo huu katika maeneo yao kwani wamepata mwanga wa kuendesha michezo kitaalam zaidi tofauti na awali ambapo hawakufahamu vema.
Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464