Washtakiwa watatu kati ya wanne walioshtakiwa kwa kosa la mauaji ya Milembe Suleiman (43), aliyekuwa mfanyakazi wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) wametiwa hatiani na kuhukumiwa adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
Mahakama imetoa adhabu hiyo baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri ambao umethibitisha kosa hilo pasipo kuacha shaka.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumanne Agosti 21, 2024 kuanzia saa 3.02 asubuhi hadi saa 5.12 asubuhi na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Geita, Kelvin Mhina.
Amesema kwa mujibu wa ushahidi, kifo cha Milembe hakikuwa cha kawaida.
Jaji Mhina amesema kuhusu nani alimuua, ushahidi upo kwenye vinasaba, ripoti ya uchunguzi, CCTV, na maelezo ya washtakiwa.
Amesema ushahidi wa DNA wa damu uliochukuliwa kwenye jambia lililotumika kumuua Milembe, matokeo yanaonyesha ni ya mwanamke.........